MAKALA: Ukosekanaji wa fidia kwa wahanga wa kesi za udhalilishaji unavyosokota mioyo yao.
NA THUREYA GHALIB- PEMBA. .
Kuna Msemo usemao Adhabu ya kaburi aijuaje maiti huu ni msemo unaofahamisha kuwa aliyefikwa na shida fulani ndiye anaejua na kufahamu shida ya jambo husika.
Au pia kuna msemo unaosema aisifuye mvua imemnyeshea,msemo huu unamana kuwa kila jambo ambalo mtu analizingumzia atakuwa aidha ana uzoefu nalo kwa namna moja au nyengine analifahamu.
Hii ni misemo inayonesha ni jisi gani Mtu anapopata matatizo unatakiwa umskilize na kumpa faraja maana yeye ndie mtu pekee anaehisi uchungu wa Jambo hilo.
Leo Katika Makala haya nimelenga kuzungumzia ni kwa namna Gani ukosekanaji wa Fidia kwa Wahanga wa Kesi za udhalilishaji unavosokota mioyo yao .
Nini maana ya malipo ya fidia?
Maana ya malipo ya fidia kikawaida fidia inarejelea malipo ya pesa yanayot...