VIJANA wajenga imani na Serekali ya Umoja wa Kitaifa.
NA ABDI SULEIMAN.
ILIKUWA ni Disemba 7/2020, Zanzibar imeandika hitoria kwa mara ya pili, baada ya mivutano mingi ya kisiasa kufuatia maalim Seif Sharif Hamad kuteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Kuteuliwa kwa Makamu wa kwanza wa Rais Maalimu Seif Sharif kutoka chama cha ACT-Wazalendo kumepunguza raghba kwa baadhi ya wananchi, huku wengine wakianza kujenga matumaini na viongozi wa juu wa serikali iliyopo madarakani.
Kama tunavojuwa vijana ndio nguvu kazi kubwa ya Taifa lolote duniani, ndio wanaotumiwa vibaya na wanasiasa wakati wote wa kampeni lakini sasa wameonyesha kujawa na furaa kufuatia kuwepo kwa serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar.
Hivi karibuni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema wakati umefika kwa waz...