Viongozi wa dini wananafasi ya kunogesha maridhiano, amani ya Zanzibar Mufti Mkuu asema amani, utulivu iwe maisha ya kila siku
NA HAJI NASSOR, PEMBA
OFISI ya Mufti Zanzibar ni moja kati ya Idara zinazomilikiwa na serikali ya Mapinduzi, ambapo miongoni mwa majukumu yake ni kusimamia, kuratibu na kutoa uamuzi ‘fat-wa’ kwa yale mambo husika.
Ofisi hii, katika kufanikisha shughuli zake imekuwa ni wadau wake mbali mbali, iwe ni wa ndani au nje ya Zanzibar, ikiwa tu wadau hao, wana malengo na maazimio yanayofanana.
Kwa mfano, ofisi hii ya Mufti kwa upande wa kisiwani Pemba imekuwa ikifanyakazi karibu mno na taasisi isiyo ya serikali ya ‘Marafi wa Zanzibar’ ‘Friend of Zanzibar’ pamoja na taasisi ya Interfarce.
Taasisi hizi, zimekuwa zikifanya shughuli mbali mbali wanazoshirikiana na Ofisi ya Mufti kwa upande wa Pemba, ili kuhakikisha, jamii ya watu wa Pemba kwa ujumla wao, wanaishi kwa amani na ...