MAKALA MAALUM: MWANAMKE JASIRI ALIEIFUFUA JUMUIYA ILIYOPOTEZA MUELEKEO NA KUPATA MAFANIKIO.
NA, AMINA AHMED MOH'D- PEMBA.
Kila aneyepanda mbegu hutarajia mavuno mazuri na pale ambapo mti ukiwa haujashuhulikiwa vizuri basi mazao yake huwa madogo na pengine yasiwe na ubora wa kuridhisha wala kuvutia.
Hivyo hivyo huwa kwa kikundi cha watu kinapoamua kuunda jumuiya au taasisi kwa vile baada ya uzazi huitajika malezi na hio pia sio kazi rahisi.
Kazi ya malezi imekuwa na changamoto zisizo hesabika kidoleni kwa taasisi na jumuiya nyingi Zanzibar na unaweza kusema nyengine zipo kwa jina tu.
Hali hii ndio inayopelekea baadhi ya wakati kusikika Msajili wa Asasi za kiraia akitaka kuzifuta baadhi ya asasi kwa vile shughuli zake hazionekani.
Moja ya taasisi ambayo kuwepo kwake kulitetereka na jamii ikawa haioni kwa vitendo shughuli ziliopelekea kuundwa k...