MAKALA: Udhalilishaji wa mitandaoni upo tumia mitandao ya kijamii kwa ungalifu.
THUREYA GHALIB PEMBA.
Kuna ule msemao TAHADHARI KABLA ATHARI au mwengine husema mzaha mzaha hutumbua usaha,hii ni misemo ya Kiswahili inayokukumbusha kuchukua tahadhari ya kitu kabla hayajakufika matatizo .
Udhalilishaji wa mitandaoni ipo kwa kiasi kikubwa katika jamii na kwa watu wa matabaka mbalimbali huwa wanapitia.
Hakuna aliekuwa salama katika dunia hii ya kidigitali ili kuepuka udhalilishaji huu,ikiwa utakuepuka wewe basi mtoto wako ama ndugu yako lazima akutane nao ,na ni jambo linaloathiri akili sana.
Kwa kitalamu Udhalilishaji huu unaitwa (cyber bulling- saiba bulling),katika nchi nyingi udhalilishaji wa mtandao haujawekea sheria bado ya kuwatia hatiani wafanyaji wa matendo haya.
(more…)