AFYA YA UZAZI SALAMA KWA WANAFUNZI WAKIKE INAHITAJI MAZINGIRA SALAMA KIPINDI CHA HEDHI
AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.
Hedhi salama ni hali ya Mwanamke au msichana aliye katika hedhi kuwa na uwezo wa kupata kifaa salama na nafuu cha kuzuia Damu, kupata Maji Safi na salama ya kujisafishia, kuwa na maliwato yenye mlango kwa ajili ya kujisitiri na kubadilishia vifaa vyake pia kupata sehemu sahihi ya kutupa au kutunzia kifaa chake baada ya kukitumia
KAMA Hiyo ndio maana halisi ya Hedhi salama bila shaka Bado kuna mengi yanahitaji kuangaliwa na wadau Serikali na wote wanaopenda Maendeleo Bora ya Afya ya Uzazi na Elimu kwa watoto wa kike.
Wadau wengi hujali Afya ya mtoto wa kike kwa kutoa Elimu ya Afya ya Uzazi kwa baadhi ya wanafunzi waliofikia Umri wa Kupata Hedhi kwa kugawa Sabuni pamoja na Taulo zakike lakini bado kuna changamoto Nyingi ambapo zisipoangalia k...