‘KINJE KUKU’ UTAMADUNI WA MICHEWENI UNAOWAHUSU WATOTO WA KIKE PEKEE
NA MARYAM SALUM, PEMBA.
UTAMADUNI wa uvaaji kanga ya shingoni, ama kwa lugha Micheweni ‘kinje kuku’ umepotea kwa kasi.
Kizazi cha sasa cha Micheweni, na hasa watoto wa kike ambao ndio walengwa wa utamaduni, wameanza kuupa kisigo.
Wakionekana, kuachana na vazi hilo, na sasa wakivaa nguo nyingine ambazo wanaona zinawastiri hasa sehemu ya kifuani.
Hiyo ni kutokana na karne ya sasa na utandawazi jinsi ulivyokua, ndipo watoto wa kike wa Micheweni takribani kwa asilimia kubwa kuacha utamaduni huo.
Vazi hili lilikua linavaliwa sana na watoto, wengi wao wanaishi vijijini, lengo hasa la kinje kuku, ni kuwastiri watoto hao wa kike sehemu ya kifuani, hasa wakianza kutanuka kifua.
Vipo vijiji vyengine vingi katika Mkoa huo ambavyo watoto wa kike walikua wanavaa vazi hilo kama utamaduni wao, ...