JAMII yahimizwa mipango matumizi bora ya ardhi
NA ABDI SULEIMAN.
MKURUGENZI wa Utafiti Tume ya Taifa ya Mipango na Mtumizi ya Ardhi Tanzania Dr.Joseph Paul, amesema bado jamii haijaona umuhimu wa mpango wa matumizi ya ardhi wakati wao ndio wanaoathirika.
Alisema kuna baadhi ya vijiji bado wananchi wanaficha madhara wanayoyapata yanayotokana na Tembo, wakihofia maeneo yao kutengwa na kuwa mapitio ya wanyamapori(Shoroba).
Mkurugenzi huyo aliyaeleza hayo Mkoani Dodoma, wakati wa ziara ya waandishi wa habari wa JET juu ya kufanya mahojiano na wakuu wa taasisi mbali mbali zinazohusika na Uhifadhi, iliyoandaliwa na JET chini ya mradi wa Tuhifadhi Maliasili Tanzania kutoka shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID).
Alisema Tembo walivyokua hatari katika maisha ya binaadamu, baadhi ya vijiji vinashindwa kutoa taarifa ya ma...