SERIKALI kupitia Wizara ya Utalii Zanzibar imeanza kuyafanyia ukarabati majengo ya kihistoria kwa lengo la kurejesha uasili wake.
NA ZUHURA JUMA, PEMBA
SERIKALI kupitia Wizara ya Utalii Zanzibar imeanza kuyafanyia ukarabati majengo ya kihistoria kwa lengo la kurejesha uasili wake, jambo ambalo litasaidia kuimarisha utalii kisiwani Pemba.
Akizungumza Chwaka Tumbe Wilaya ya Micheweni, Matibu wa Idara ya Makumbusho Pemba Khamis Ali Juma alisema kuwa, majengo ya kihistoria yamekuja na sura mpya ya utalii, hivyo yakifanyiwa maboresho yatarudi katika uasili wake.
Alisema kuwa, Idara yao ina dhamira ya kurejesha uasili wa majengo ya kihistori kwa lengo la kuimarisha utalii na kurudisha historia kamili, ili vizaji vijavyo viweze kujua.
“Tunafanya ukarabati lakini tunafuata vile vile yalivyo majengo haya na tunatumia zana zile zile, ili yawepo katika uasili wake, hivyo tunaamini kwamba wataimarisha utalii kwani ma...