Sekta binafsi nazo zina wajibu kusaidia uhifadhi wa bayoanuai na kulinda mapitio ya wanyamaporo-Mkurugenzi CHEMCHEM Walter Pallangyo
NA ABDI SULEIMAN.
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya CHEMCHEM Walter Pallangyo, amesema wajibu wa sekta binafsi katika kusaidia uhifadhi wa bayoanuai na kulinda mapitio ya wanyamaporo (shoroba), ni kuhakikisha jamii inayozunguka eneo lililohifadhiwa wanakua na uwezo wa kutengeneza vyanzo vyao vya mapato, ambavyo vitawasaidia kufanya ujangili wa wanyamapori na uharibifu wa mazingira.
Alisema katika kutilia mkazo hilo Chechem, imelazimika kutengeneza vikundi vya akinamama vya kuweka na kukopa (vicoba), wanawake hukutana na kuzungumzia masuala ya uhifadhi na kuweka hakiba zao na kupata mikopo.
Alifahamisha kuwa wameweza kusaidia ukarabati wa madarasa na kujenga mapya, kwa skuli ambazo zimetawanyika katika shoriba ili kuwasaidia watoto, kupata elimu na kuacha kutapakaa mitaani na...