Sangaiwe wapongeza uwekaji wa kamera maalumu katika hifadhi ya Wanyama Burunge
NA ABDI SULEIMAN, BABATI.
WANANCHI wa Kijiji cha Sangaiwe Wilaya ya Babati Mkoa wa Mnyara, wamesema mradi wa uwekaji wa kamera maalumu katika hifadhi ya Wanyama Burunge, utaweza kuwasaidia kupata mazao yao mbayo walikuwa wakiyakosa kutokana na kuvamiwa na wanyama.
Walisema kamera hizo zitaweka katika maeneo maamulu, ambayo wanyama wakipita kuingia katika mashamba ya wakulima wataonekana moja kwa moja na walinzi kwenda kumfurusha.
Wakizungumza na timu ya waandishi wa habari za Mazingira kutoka (JET), waliotembelea hifadhi wanyama Burunge shuruba ya kwakuchinja, kupitia mradi wa USAID “Tuhifadhi Maliasili”, unaotekelezwa na Chama cha Waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET).
Mmoja ya wananchi hao Anastazia John Mwanso (50), alisema mradi huo ni mzuri kwani utaweza kuwa...