Saturday, December 28

MAZINGIRA

Utekelezaji wa kampeni kabambe ya mazingira washika kasi.
MAZINGIRA

Utekelezaji wa kampeni kabambe ya mazingira washika kasi.

  Na Lulu Mussa -Dar es Salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo leo tarehe 10 Disemba, 2021 amekabidhi Mpango Kazi wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira na Mwongozo wa Tuzo ya Taifa ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kwa wajumbe wa Kamati Maalumu ya Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mohammed Khamis Abdulla, amesema Lengo la Kampeni hiyo ni kuelimisha na kuhamasisha ushiriki wa jamii na uwajibikaji wa mamlaka za usimamizi katika hifadhi na usafi wa mazingira ili kuleta ustawi wa jamii ya watanzani...
JET yatoa elimu ya uhifadhi , maliasili kwa waandishi wa habari Tanzania
ELIMU, MAZINGIRA

JET yatoa elimu ya uhifadhi , maliasili kwa waandishi wa habari Tanzania

NA ABDI SULEIMAN. MWENYEKITI wa Chama cha Waandishi wa habari za Mazingira Tanzania, (JET) Dr.Ellen Otaru, amesema kazi kubwa iliyopo ni kutoa elimu na ushirikishwaji wa vijana na wanawake, katika ulinzi na uhifadhi wa mazingira na maliasili kwa maendeleo endelevu. Alisema matumizi mabaya ya mazingira hupelekea wanyama na viumbe mbali mbali kupotea na baadhi yao kufariki, hayo yanatokana na matumizi mabaya ya mazingira yanayofanywa na binaadamu. Akizungumza katika mkutano uliowashirikisha waandishi wa habari za uhifadhi, uwindaji haramu wa wanyamapori na usafirishaji, kupitia mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, unaotekelezwa na Chama cha Waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET). Alisema asilimia 40% ya watanzania ni Vijana ndio tegemeo la taifa, huku miundombinu ya ...
JET yawataka waandishi wa habari za uhifadhi kuyashirikisha makundi yote
Biashara, Kitaifa, MAZINGIRA

JET yawataka waandishi wa habari za uhifadhi kuyashirikisha makundi yote

NA ABDI SULEIMAN. CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), kimewataka waandishi wa habari za uhifadhi, uwindaji haramu na usafirishaji wa wanyamapori Tanzania, kuhakikisha wanayashirikisha makundi yote wakati wa kuandika habari hizo. JET imesema wakati umefika katika kuandika habari hizo kuyashirikisha makundi yote yanayohusika ikiwemo wanawake, watoto, wazee na Vijana. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa habari za Mazingira Tanzania (JET) John Chikomo, wakati akifungua mafunzo juu ya kuongeza uwelewa wa waandishi wa habari, juu ya biashara ya wanyamapori kubadilisha tabia ya jamii kuelekea utumiaji wa wanyamapori haramu, kupitia taasisi ya TRAFFIC ya Afrika Mashariki. Alisema waandishi wananafasi kuwa kuyatumia makundi hayo katika haba...
TUCHUKUE JUHUDI ZA MAKUSUDI KUYATUNZA MAZINGIRA – MHE.OTHMAN
MAZINGIRA

TUCHUKUE JUHUDI ZA MAKUSUDI KUYATUNZA MAZINGIRA – MHE.OTHMAN

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema pamoja na juhudi za Serikali katika kuhamasisha utunzaji wa mazingira nchini, kunahitajika juhudi za pamoja ili kukabiliana na tishio kubwa la athari za mabadiliko ya tabianchi. Mheshmiwa Othman ameyasema hayo leo, Kiungoni, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ziara yake ya kimazingira, akitembelea na kukagua maeneo mbali mbali yaliyopatwa na athari za kimazingira zilizotokana na mabadiliko ya tabianchi. Akiongea na wananchi wa kijiji hicho, Mheshimiwa Othman amesema Serikali inaelewa na imeamua kushughulikia changamoto za mazingira, bali jambo la msingi ni mashirikiano ya wananchi wote katika kuyanusuru na kuyaendeleza. Mheshimiwa Othman ametoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa utu...
TAASISI YA BRIGHT ENVIRONMENT YAPONGEZWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Kitaifa, MAZINGIRA

TAASISI YA BRIGHT ENVIRONMENT YAPONGEZWA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

    Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Hamad Hassan Chande mwishoni mwa wiki ameshiriki katika zoezi la upandaji miti lililoandaliwa na Taasisi ya Bright African Environment Development Group na kusisitiza kuwa ni kitendo cha kuigwa na kupongezwa na hivyo kutoa rai kwa jamii kuiga mfano huo Mhe. Chande ameupongeza uongozi wa Taasisi hiyo inayomiliki Shule ya Bright African kwa kusimamia mazingira kwa vitendo hasa uanzishaji wa vitalu vya miche ya miti na matunda kwa wanafunzi wake. Amesema sasa hivi jamii inakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa Mazingira ambao umechangia matatizo mengi yanayoathiri maendeleo ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na upungufu wa umeme na mgao wa maji. “Mmefanya jambo jema sana kuanza kuwapa ujuzi wan...