Sunday, November 24

MAZINGIRA

TAARIFA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) MHE. SELEMANI JAFO WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI AKIELEZEA MAFANIKIO YA MUUNGANO NA MAZINGIRA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA
Kitaifa, MAZINGIRA

TAARIFA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) MHE. SELEMANI JAFO WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI AKIELEZEA MAFANIKIO YA MUUNGANO NA MAZINGIRA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA

TAARIFA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) MHE. SELEMANI JAFO WAKATI WA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI AKIELEZEA MAFANIKIO YA MUUNGANO NA MAZINGIRA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA Ndugu Wanahabari, Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana hapa leo tukiwa na afya njema ili sote kwa pamoja tuweze kuwapasha wananchi taarifa muhimu. Tunatambua mchango wenu katika kuelimisha na kuwapasha habari wananchi kuhusu mchango wa Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu masuala ya Muungano na Mazingira ambayo imepewa jukumu la kuyasimamia. Ndugu Wanahabari, Kama tunavyofahamu sasa hivi tuko katika kipindi cha maandalizi ya kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara itakapofika tarehe 9 ...
​Jafo: Suala la mabadiliko ya tabianchi siyo la kufikirika tena
Kitaifa, MAZINGIRA

​Jafo: Suala la mabadiliko ya tabianchi siyo la kufikirika tena

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo amesema suala la Mabadiliko ya Tabianchi lipo na madhara yake yanaonekana katika sehemu mbalimbali kwenye nchi yetu ya Tanzania. Ameyasema hayo leo Novemba 14, 2021 wakati wa mbio za kuhamasisha utunzaji wa mazingira (MAZINGIRA MARATHON) zilizofanyika kwenye viwanja vya Green Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zililenga kuhamasisha utunzaji wa mazingira kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi. Mhe. Jafo amesema dunia kwa sasa ipo hatarini kutokana na mabadiliko ya Tabianchi na kuna baadhi ya maeneo yamesha athiriwa na athari za mabadiliko hayo kama kutoweka kwa Kisiwa cha Kifungu. Mhe. Jafo ameongeza kuwa kina cha maji kinazidi kuongezeka mfano kwenye visiwa vya Pemba hali inayopelekea uwe...
TANZANIA ILIVYOSHIRIKI KATIKA MKUTANO WA 26 WA MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI ULIOFANYIKA, GLASGOW, USKOCHI- WAZIRI JAFO
Kitaifa, MAZINGIRA

TANZANIA ILIVYOSHIRIKI KATIKA MKUTANO WA 26 WA MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA WA MABADILIKO YA TABIANCHI ULIOFANYIKA, GLASGOW, USKOCHI- WAZIRI JAFO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Selemani Jafo amekutana na wanahabari jijini katika Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)jijini Dar es Salaam na kutoa taarifa ya yaliyojiri katika Mkutano wa 26 wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika mjini Glasgow nchini Uskochi. Amesema kuwa Mafanikio ya mkutano huo yatadhihirika zaidi pale ambapo mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huu yatatekelezwa kwa vitendo maazimio na makubaliano yaliyofikiwa lakini zaidi utekelezaji wa mikakati ya kitaifa. Aidha aliongeza kuwa ili kufanikiwa katika hili anatoa wito kama ifuatavyo:Watendaji katika Wizara, Taasisi na Sekta binafsi watekeleze majukumu yao katika kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya hatua za kuchukua yanayozihusu Wi...
COP26: Maneno ya kukwepa na maelewano ya makaa ya mawe, lakini mkataba unaonyesha kuendelea
Kimataifa, MAZINGIRA

COP26: Maneno ya kukwepa na maelewano ya makaa ya mawe, lakini mkataba unaonyesha kuendelea

  CHANZO CHA PICHA,REUTERS Maelezo ya picha,Waandamanaji karibu na mkutano wa wa COP, wakiandamana kuunga mkono waathiriwa wa uchimbaji mafuta Ingawa Mkataba wa Hali ya Hewa wa Glasgow ni jaribio kubwa la kudhibiti ongezeko la joto duniani, mzozo wa dakika za mwisho juu ya makaa bila shaka umegubika mpango huo. India iliungana na China katika kushinikiza kupunguzwa kwa ahadi hii kuu, ikisisitiza "kupunguza" badala ya "kuondoa". Ilikuwa onyesho la ujasiri la msuli wa kisiasa wa kijiografia ambao uliacha nchi zinazoendelea na mataifa ya visiwa na chaguo kidogo ila kwenda sambamba na mabadiliko. Mkataba huo mpya unakuja siku chache tu baada ya mafanikio mengine mashuhuri ya China. Jumatano iliyopita shirika la habari ...
Uchafuzi wa hewa wachochea nimonia: Oksijeni yahitajika
afya, MAZINGIRA

Uchafuzi wa hewa wachochea nimonia: Oksijeni yahitajika

Kwa mujibu wa UNITAID ripoti ya mwaka 2019 inaonesha nusu ya vifo vyote vya watoto wenye umri wa chini ya mwaka mmoja katika nchi za Nigeria, India, Pakistan, Ethiopia na Niger vimesababishwa na ugonjwa mmoja wa Nimonia. Nimonia, ni ugonjwa wa kupumua unaoathiri mapafu ukisababishwa na maambukizi ya virusi, vimelea, na fangasi ambapo hata kabla ya janga la COVID-19, ulikuwa ukisababisha vifo vingi ulimwenguni. Ndio maana shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa tiba nafuu, UNITAID limetoa wito kwa washirika wake katika ngazi zote, kuongeza fedha ili kupunguza vitokanavyo na nimonia kama anavyoeleza Robert Matiru, Mkurugenzi wa Programu wa shirika hilo. “Tunahitaji kujitolea zaidi kisiasa katika ngazi zote. Tunahitaji uwekezaji wa ziada, hasa kwa bidhaa za kiaf...