NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, amewasihi wananchi kuendelea kuitunza bahari, kwani bahari ikiwa salama itapelekea kukuza uchumi wa bahari, ikizingatiwa dhamira kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutumia bahari katika uchumi.
Alisema mazingira bahari kuendelea kubakia salama ni jambo la muhimu, kwani kuna viumbe bahari na vinahitaji bahari na sisi wenyewe tunahitaji bahari, hivyo wadau na wananchi wanakila sababu kuhakikisha wanaendelea kuelimisha jamii.
Mkuu huyo wa Mkoa aliyaleza hayo katika ukumbi wa baraza la Wawakilishi Zamani Wete, wakati akizungumza na wadau wa bahari hivi karibuni.
Aidha alisema ni muhimu kwa kila mmoja kusimamia mazingira ya usalama wa bahari, kwani mikakati mbali mbali inaendelea kufanywa ili ku...