Vijana tumieni fursa za mazingira kujinufaisha
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib amesema, ujumbe wa siku ya vijana duninia mwaka huu, umeonyesha umuhimu wa elimu na utunzaji wa mazingira kwa vijana, hivyo ni wajibu wao kuufanyia kazi kwa vitendo.
Alisema, iwapo vijana watapatiwa elimu na ujuzi wa mazingira kwa ajili ya kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, wataweza kusaidia sana kutunza mazingira yaliyowazunguka na kuwanufaisha.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni Mkuu huyo alisema fursa zinazotokana na mazingira ni nyingi, hivyo kuna haja kwa vijana kuhakikisha wanazitumia ipasavyo ili kujikomboa.
Alisema kuwa, kaulimbiu ya siku hiyo ambayo ni ‘Elimu na Ujuzi wa kijani kwa vijana kwa maendeleo endelevu’ inahimiza vijana kuzitumia fursa za...