Suala la uharibifu wa mazingira Mtambwe Kusini bado changamoto.
NA ABDI SULEIMAN.
WANANCHI wa Shehia ya Mtambwe Kusini Wilaya ya Wete, wamesema suala la uharibifu wa mazingira juu ya ukataji wa miti katika shehia yao, limekua likiwaumiza kichwa licha juhudi mbali mbali wanazozichukua.
Walisema hali hiyo imepelekea maji ya bahari kuingia katika mashamba ya kilimo, jua kua kali, kukosekana kwa mvua katika shehia yao kitu ambacho hawajakizowea.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wananchi wa shehia hiyo, walisema wanaofanya uharibifu huo ni vijana kutoka ndani ya shehia kwa kushirikiana na wageni, kutoka shehia za jiran zikiwemo ndagoni, Mchanga mdogo, Jojo na Micheweni.
Salum Hamid Kombo mkaazi wa Mtambwe Kusini, alisema uharibifu wa mazingira upo kwa kiasi kikubwa, kwani miti inakatwa kwa ajili upigaji wa mkaa, majenzi,...