Sunday, November 24

MAZINGIRA

Mwenge wa uhuru watua Pemba, waanza kwa kishindo wilaya ya Wete
Kitaifa, MAZINGIRA

Mwenge wa uhuru watua Pemba, waanza kwa kishindo wilaya ya Wete

NA HAJI NASSOR, PEMBA MWENGE wa uhuru umewasili kisiwani Pemba, ukitokea Mkoa wa kaskazini Unguja, tayari kwa ajili ya kukimbizwa katika wilaya nne za Pemba, samba mba na ufunguzi wa miradi kadhaa, ikiwemo ya maendeleo kisiwani humo. Mwenge huo umepokelewa jana, katika uwanja wa ndege wa Karume Pemba, ambapo wananchi wa mikoa miwili ya Pemba, wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib, wamejumuika. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa kaskazini Unguja Ayoub Mohamed Mahamoud, alisema mwenge huo ukiwa mkoani mwake, ulizindua miradi minane ya maendeleo na program nne, yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 14.4. Alisema wakimbiza mwenge, walitoa ujumbe kwa wananchi, ukiwemo suala la uhifadhi na utunzaji wa mazingira, lishe na kupinga r...
Nguvu ya pamoja inatakiwa  katika kusimamia  katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.
MAZINGIRA

Nguvu ya pamoja inatakiwa katika kusimamia  katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini kuongeza nguvu zaidi katika kusimamia utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini. Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo mara baada ya kuongoza zoezi la kufanya usafi katika soko kuu la wamachinga mjini Dodoma ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani leo tarehe 5 Juni 2023. Amesema ni lazima kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wanaokiuka maagizo hayo pamoja na kuwataka watendaji wote wanaohusika kusimamia kwa karibu uzalishaji na matumizi ya mifuko mbadala.   Makamu wa Rais ameongeza kwamba ni vema kuhakikisha mifuko yote ina...
TUONGEZE JITIHADA ZA KUFANYA UTAFITI WA KUTOKOMEZA MIMEA VAMIZI- JENARELI VENANCE MABEYO.
hifdhi na utalii, MAZINGIRA

TUONGEZE JITIHADA ZA KUFANYA UTAFITI WA KUTOKOMEZA MIMEA VAMIZI- JENARELI VENANCE MABEYO.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NCAA Jenerali Venance Mabeyo (mstaafu) ametoa rai kwa wataalam wa masuala ya uhifadhi kuongeza jitihada na mbinu mbalimbali za kiutafiti zitakazosaidia kupunguza changamoto za mimea vamizi katika maeneo ya hifadhi. Jenerali Mabeyo ametoa rai hiyo wakati wa ziara ya Bodi hiyo katika Kreta ya Ngorongoro kukagua juhudi zinazofanywa na uongozi wa NCAA kukabiliana na athari za mimea vamizi iliyoathiri baadhi ya maeneo ya hifadhi hiyo. Akiwa katika eneo hilo Jenerali Mabeyo ameona zaidi ya ekari 257 zilizokuwa na mimea vamizi ambazo tayari zimefyekwa kabla ya mbegu zake kukomaa. Amebainisha kuwa  hapo awali kulikuwa na tatizo la uelewa wa namna ya kupambana na mimea hiyo lakini kwa sasa njia ya kufyeka na kuchoma moto mimea yenye mbegu ambazo h...
IPDO yapanda miti 1,000 Pemba.
hifdhi na utalii, MAZINGIRA

IPDO yapanda miti 1,000 Pemba.

 SAID ABRAHMAN-PEMBA. MKUU wa Wilaya ya Wete Dkt, Hamad Omar Bakar ameungana na wana jumuia ya IPDO ya Kinyasini Wete pamoja na wananchi wa Shehia hiyo na Vitongoji vyake katika uzinduzi wa upandaji miti katika Skuli ya Sekondari Kinyasini. Akizungumza baada ya zoezi hilo,Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi hao kuilinda miti hiyo ili lengo lake liweze kufikiwa. Dkt, Hamad alifahamisha kuwa lengo la upandaji miti ni kuhifadhi mazingira, hivyo aliwasisitiza wananchi hao kuendelea kupanda miti kwa wingi katika maeneo yao ili kuweza kuzuia mmong'onyoko wa ardhi pamoja na kuzuia upepo ili usiweze kuharibu vipando vyao. Sambamba na hayo aliwataka wananchi  kutoruhusu kufungwa kwa mifugo ya aina yeyote katika shamba hilo na ni vyema kuweka utaratibu mzuri ambao utaweza kutoa...
WAKATI NI SASA WA MAGEUZI KULINDA FEDHA ZA UMMA – DKT MWINYI.
Biashara, Kitaifa, MAZINGIRA

WAKATI NI SASA WA MAGEUZI KULINDA FEDHA ZA UMMA – DKT MWINYI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dokta Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kwamba Serikali zote Mbili, ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zitaendelea kuungamkono Shughuli za Ukaguzi wa Ndani, ili kulinusuru Taifa kutokana na vihatarishi dhidi ya Raslimali na Fedha za Umma. Dokta Mwinyi ameyasema hayo leo kupitia Hotuba yake iliyowasilishwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, wakati wa Hafla ya kufungua Mkutano wa Pili wa Utawala wa Sekta ya Umma na Ukaguzi wa Ndani, ulioandaliwa na Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA) huko Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege, Mkoa wa Mjini-Magharibi, Unguja. (more…)