ZEMA ZATEKETEZA TANI TATU NA KILO 450 ZA VIFUKO VYA PLASTIKI.
NA ABDI SULEIMAN.
MAMLAKA ya Usimamizi wa Mazingira Pemba (ZEMA), imefanikiwa kuteketeza kwa moto tani tatu (3) na kilo 450 za vifuko vya plastiki vikiwa na thamani zaidi ya shilingi Milioni 40.5.
Zoezi hilo la utekeletezaji wa vifuko vya Plastiki, limefanyikwa huko Vitongoji kwareni liwa limesimamiwa na viongozi mbali mbali wakiwemo mahakimu, ZAECA na taasisi nyengine.
Akizungumza na waandishi wa habari mara, baada ya kumalizika kwa zoezi la uchomaji wa vifuko hivyo, Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Kwanza Rais Ahmed Abubakar, alisema fedha nyingi imepotea katika vifuko hivyo, jambo ambalo linalopelekea umaskini kwa wahusika.
Aliwasihi wananchi kufanya biashara za halali ambazo serikali na wananchi inazikubali, ambazo ziko salama na zinaweza...