SMZ itaendelea kuipa kipaombele Sekta ya Michezo hasa michezo Jumuishi.
Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuipa kipaombele Sekta ya Michezo hasa michezo Jumuishi ili kutoa fursa kwa watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu kujumuika pamoja katika kujifunza na kushiriki katika michezo mbali mbali pasipo na utenganishi miongoni mwao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduziu Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo katika Hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati akifungua Warsha ya Kimataifa kuhusu Skuli na Michezo Jumuishi katika Ukumbi wa Hotel Verde Mtoni jijini Zanzibar.
Amesema kuwepo na Michezo Jumuishi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kutasaidia kukuza na kuhuisha ushiriki wa watu wenye ulemavu hususan ulemavu wa akili kwenye mashindano mbali mbali ya mi...