YANGA ya banwa mbavu na timu ya Daraja la kwanza Pemba
KLABU ya soka ya Yanga imeshindwa kutamba mbele ya Jamhuri inayoshiriki ligi daraja ;la kwanza Taifa Pemba, kwa kulazimishwa sare isiyokuwa na magoli katika mchezo wa mashindano ya kombe la Mapinduzi uliochezwa usiku wa kuamkia jana.
Mchezo huo ambao wengi wa mashabiki waliokuwepo hapo hawakuweza kuamini na kilichotokea ulichezwa katika uwanja wa Amaan mjini Unguja.
Katika mchezo huo ambao ni wa ufunguzi mgeni rasmi alikuwa ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman, ambae aliungana na wadau wa mchezo huo waliofika uwanjani hapo.
Miamba hiyo ambayo ilikuwa ikishambuliana kwa zamu ilienda mapumziko wakiwa hakuna ambae alieouna mlango wa mwenziwe.
Kipindi cha pili kilianza na mashambulizi kama kawaida yakaendelea, huku Yanga ambayo ilijaribu kuliandama sana lango la wapinzani...