Mahafali ya 10 ya skuli ya maandalizi Star yafana.
MKURUGENZI wa Elimu ya Msingi na Maandalizi kutoka Baraza la Mji Chake Chake Makame Pandu Khamis, amewataka wazazi au walezi kuhakikisha wanaitekeleza kwa vitendo mikaba wanayopewa skuli, wakati wanapokwenda kuwaandikisha watoto wao ili kuepuka migogoro inayotokea baadae.
Alisema kumekua na tabia ya wazazi kutokuifuata kimilifu mikataba hiyo, baada ya watoto wao kukubaliwa katika skuli walizowapeleka.
Mkurugenzi huyo aliyaeleza hayo wakati wa mahafali ya 10 ya skuli ya maandalizi Star Nursery school iliyopo kichungwa Wilaya ya Chake Chake, pamoja na kuzungumza wazazi na walezi wa watoto.
Alisema iwapo wazazi watashindwa kutekeleza kwa vitendo mikataba wanayopewa skuli, skuli hizo zitakosa maendeleo ikizingatiwa hazina bajeti wala ruzuku kutoka serikalini.
“Niv...