Monday, January 27

Sheria

TAMWA-Zanzibar yataka uwazi na mawasiliano yaendelee kwenye kesi za ukatili.
Sheria

TAMWA-Zanzibar yataka uwazi na mawasiliano yaendelee kwenye kesi za ukatili.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: TAMWA-Zanzibar yataka uwazi na mawasiliano yaendelee kwenye kesi za ukatili. CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kinaziomba taasisi zinazosimamia masuala ya sheria na upatikanaji wa haki likiwemo Jeshi la Polisi, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka na Mahakama kuendeleza uwazi na mawasiliano katika kushughulikia kesi za ukatili wa kijinsia ikiwemo mauaji. Hivi karibuni Mahakama Kuu Zanzibar ilitoa taarifa kuwa imemuhukumu mshitakiwa Haji Jaha Issa (37) kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua kwa makusudi Hajra Abdallah Abdallah (21) ambapo alimchoma kisu kifuani, ubavuni na tumboni. Taarifa hiyo ilitaja kuwa hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Rabia Hussein Mohammed ambaye aliridhishwa na ushahidi uliotolewa katika mauaji hayo yal...
Wasaidizi wa sheria wafutiwa ada Zanzibar-Waziri Haroun
Sheria

Wasaidizi wa sheria wafutiwa ada Zanzibar-Waziri Haroun

  NA ABDI SULEIMAN, PEMBA. WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman, ametangaza rasmin kufuta ada ya usajili kwa wasaidizi wa sheria. Hayo aliyasema wakati akifunga jukwaa la tatu la mwaka la msaada wa kisheria huko katika ukumbi wa chuo cha utalii Maruhubi Unguja. Alisema ameamua kuondosha ada hiyo, ili kuwaondoshea gharama katika utendaji wao wa kuwasaidia wananchi katika changamoto zinazowakabili. Haroun alisema ufutaji wa ada hiyo, kwa sasa unawahusu watoa msaada wa kisheria wanaojisajili mmoja mmoja wakiwemo wasaidizi wa sheria, mawakili, mavakili na wanasheria ambao hujisajili kama watoa msaada wa kisheria. “Nafahamu kuwa wasaidizi wa sheria mnalipa ada ya shilingi 20,000 kuanzia sasa natangaza rasmin kuifuta ...
Zanzibar imekuwa mfano bora utoaji huduma za msaada wa kisheria-LSF.
Sheria

Zanzibar imekuwa mfano bora utoaji huduma za msaada wa kisheria-LSF.

    NA ABDI SULEIMAN, PEMBA. MWAKILISHI kutoka taasisi ya LSF Tanzania Wakili Alphonce Guru, amesema Zanzibar imejidhihirisha kuwa mfano bora, kwa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria, sio ndani tu hata nje ya Tanzania na Afrika Mashariki. Wakili huyo alisema, hilo lilijihidhirisha Agosti 8 Mwaka huu, katika mkutano mkubwa uliowashirikisha wadau kutoka Serikalini na watoa msaada wa kisheri kutoka Zanzibar na nje ya Tanzania, ulionesha wazi jinsi gani Zanzibar imepiga hatua katika utoaji wa huduma hiyo. Aliyasema hayo wakati akitoa salamu za taasisi ya LSF, katika Jukwaa la Tatu la Mwaka la Msaada wa Kisheria Zanzibar 2023, lililoandaliwa na idara ya katiba na msaada wakisheria Zanzibar kwa Ufadhili wa LSF NA UNDP, nakufanyika katika chuo cha Utalii Maruh...