Wamiliki wa vyombo vya utangazaji wametakiwa kufuata sheria zilizowekwa na Tume.
KATIBU Mtendaji wa Tume ya Utangazaji, Suleiman Abdulla Salim, amesema wakati umefika kwa wamiliki wa vyombo vya utangazaji kufuata sheria zilizowekwa na Tume sambamba na kuhakikisha wanajisajili ili kufanya kazi zao kwa uadilifu na umakini zaidi ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofsini kwake Kilimani, Katibu Suleiman alisema ukaguzi wa hivi karibuni uliofanywa na Tume umebaini wapo baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari vya utangazaji wanafanya kazi zao bila ya kufuata sheria na miongozo jambo hilo ni kinyume na matakwa ya serikali.
“Katika tathimini yetu fupi iliyofanywa hivi karibuni tumebaini kuwepo kwa baadhi ya vituo vya utangazaji hasa vya maudhui ya mtandaoni (online tv) zimeanzishwa bila ya kufuata utaratibu hivyo Tume inatoa ...