Wadau watoa maoni juu ya rasmi ya sera ya msaada wa kisheria
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
WADAU wa Sheria Kisiwani Pemba, wamesema tatizo kubwa lililopo katika Visiwa vya Zanzibar ni kutunga Sheria nyingi, baadae wananchi wanashindwa kutekeleza yale ambayo yanatakiwa.
Wakichangia katika Mkutano wa kukusanya maoni juu ya rasimu ya sera ya msaada wa kisheria, ulioandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wakisheria Zanzibar na kufanyika mjini Chake Chake.
Mmoja ya wadau walichangia rasimu ya sera hiyo, Yussuf Abdalla Ramadhani kutoka jumuia ya KUKHAWA, alisema shida iliyopo ni utekeleza wa Sheria, licha ya Zanzibar kuwa na sheria nyong..
Alisema kuwa Sheria, kanuni zimekuwa zikitungwa lakini utekelezaji umekuwa ukisuasua, jambo ambalo linaleta sitofahamu kwa jamii.
Nae Massoud Ali...