Jamii bado inahitaji elimu ya msaada wa kisheria
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.
AFISA Mdhamini Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi na Utawala Bora Pemba Halima Khamis Ali, amesema wasaidizi wa sheria bado wanakazi kubwa sana ya kuisaidia jamii, licha ya mafanikio kadhaa walioyapata.
Alisema bado katika jamii kuna watu hawafahamu chochote mpaka leo, juu ya masuala ya kisheria changamoto hiyo ni kubwa hali inayopelekea kukumbwa na mikasa mbali mbali.
Aidha aliyataja baadhi ya matukio yanayotokea ni Udhalilishaji, madawa ya kulevya, dhuluma na ukatili wa kijinsia, watoa msaada wakisheria ndio wakuisaidia jamii kwa kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha haki inapatikana na kuonekana.
Mdhamini Halima aliyaeleza hayo wakati akifungua mkutano wa siku moja, wa Nusu Mwaka wa wahusika wa msaada wa Kisheria, ulioandaliwa ...