WAFANYAKAZI wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, wametakiwa kuendelea kulinda nidhamu na heshima ya kazi.
RAIYE MKUBWA – WVUSM.
WAFANYAKAZI wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba, wametakiwa kuendelea kulinda nidhamu na heshima ya kazi kwa kutozungumzia siasa wakiwa sehemu ya kazi, pamoja na kuacha kujiingiza katika makundi ambayo mwisho wake yatapelekea kuingia matatizoni wakati huu wa kuelekea Uchaguzi.
Hayo yameelezwa na Afisa Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Fatma Hamad Rajab, alipokua akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara hiyo katika Ukumbi wa Mkutano wa Wizara ya Fedha na Mipango Gombani Wilaya ya Chake Chake.
Alisema baada ya uchaguzi serikali inaendelea, aliwataka kuendelea kulinda heshima nidhamu ya kazi panoja na kutokujiingiza katika mambo yasiowahusu.
Aidha, amewasisitiza wafanyakazi hao kutokubali kutumiwa vibaya...