Friday, December 27

Sheria

Mashahidi waingia mitini Pemba, wasababisha kesi ya ubakaji kuondolewa
Kitaifa, Sheria, Wanawake & Watoto

Mashahidi waingia mitini Pemba, wasababisha kesi ya ubakaji kuondolewa

IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA Mahakama ya Mkoa Wete imeiondoa kesi namba 75 ya mwaka 2019 iliyokua inamkabili kijana Khamis Abdalla Khamis mwenye miaka 35 aliyetuhumiwa kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka kumi baada ya mashahidi kutofika Mahakamani. Akitoa uamuzi huo Mrajisi wa Mahakama kuu Pemba Abdul-razak Abdul-kadir Ali amesema, analiondosha shauri hilo chini ya kifungu cha 103 (9) cha sheria nambari 7 ya mwaka 2018. “Kifungu hiki kinanipa uwezo wa kuliondosha shauri ikiwa mashahihdi wameshindwa kufika mahakamani”, alisema Mrajis huyo. Alisema kuwa, upande wa mashitaka unaweza kulifungua tena shauri hilo iwapo watawapata mashahidi na na kuwapeleka mahakamani. “Upande wa mashitaka mtakapopata mashahidi wa kesi hii basi mnaweza kulirudisha tena lakini kwa leo nimelio...
Mahakama yamrejesha uraiani aliyedaiwa kumuingilia mlemavu Pujini
Kitaifa, Sheria, Wanawake & Watoto

Mahakama yamrejesha uraiani aliyedaiwa kumuingilia mlemavu Pujini

IMEANDIKWA NA HAJI NASSOR, PEMBA MAHAKAMA ya mkoa Chake Chake, imemuachia huru, kijana Abdalla Khatib Abdalla miaka 25 wa Pujini, aliyekuwa akituhumiwa kumuingilia mwanamke mwenye ulemavu wa akili, baada ya mahakama hiyo kubaini utata juu ya eneo alililodaiwa kuingiliwa mwanamke huyo. Hakimu wa mahakama hiyo Luciano Makoye Nyengo, alisema kuwa, amelazimika kumuachia huru mtuhumiwa kwa vile, shahidi mmoja alidai mwanamke huyo aliingiliwa kichani tena chini ya Muwembe. Alisema, ilipofika wakati wa shahidi muathirika ambae ana ulemavu wa akili, aliimbia mahakama hiyo kuwa, aliingiliwa na mtuhumiwa ndani ya nyumba eneo la Pujini na sio kichakani. “Shahidi mmoja alidai kuwa, tukio la kuingiliwa kwa mwanamke huyo lilifanyika kichakani, ingawa alipokuja muathirika wa tukio, aliiel...