Friday, January 31

Sheria

VIDEO: UNDP KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA KUISAIDIA  JAMII JUU YA DHANA YA UTAWALA BORA .
ELIMU, Kitaifa, Sheria

VIDEO: UNDP KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA KUISAIDIA JAMII JUU YA DHANA YA UTAWALA BORA .

NA KHADIJA KOMBO - PEMBA. Afisa  Mdhamini Ofisi ya Rais katiba sheria  Utumishi wa umma na Utawala bora Halima Khamis Ali Amezitaka jumuiya zisizo za Kiserikali  kuendelea kutoa mashirikiano katika   kuelimisha jamii  juu ya haki za binaadamu na misingi ya utawala bora ili kuendeleza   mshikamano  na Amani iliopo nchini  . Akizungumza na wanaasasi za kiraia Kisiwani Pemba wakati akifungua mafunzo  juu ya haki za binaadamu na Utawala Bora  huko katika ukumbi wa Kiwanda cha makonyo Pemba amesema utawala bora ndio kila kitu katika nchi kwani kukosekana kwake  huashiria ufunjivu wa amani na kurudisha nyuma juhudi za maendeleo. Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa uwezeshaji wa sheria na upatikanaji wa haki kutoka shirika la kimataifa la  UNDP kanda ya Zanzibar  Gramalied  amesema...
ZANZIBAR KUANZISHA KITUO CHA UTATUZI WA MIGOGORO NJE YA MAHKAMA.
Sheria

ZANZIBAR KUANZISHA KITUO CHA UTATUZI WA MIGOGORO NJE YA MAHKAMA.

Picha na Faki Mjaka. ZANZIBAR. Serikali kupitia Afisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar ipo mbioni kuanzisha Kituo cha Utatuzi wa Migogoro nje ya Mahkama (ADR Center) pamoja na Sheria zinazosimamia uanzishwaji na uendeshaji wa Kituo hicho. Kukamilika kwa Kituo hicho kutasaidia kutatuliwa kwa migogoro kwa haraka, na kinatarajiwa kuchochea zaidi ongezeko la Wawekezaji wanaokuja Zanzibar kwa vile Wawekezaji hao watakuwa na amani na uwekezaji wao nchini. Naibu MWANASHERIA Mkuu ZANZIBAR Shaaban Ramadhan Abdalla ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa kupokea maoni kuhusu Rasimu ya uanzishwaji wa Kituo hicho huko katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi hiyo Mazizini uliohudhuriwa na Wataalam wa Sheria kutoka katika Taasisi za Serikali na binafsi nchini. Naibu Shaaban amesema Sher...
Watendaji wa Mahkama Kisiwani Pemba watakiwa kujiepusha na Rushwa na uhujumu wa uchumi.
Sheria

Watendaji wa Mahkama Kisiwani Pemba watakiwa kujiepusha na Rushwa na uhujumu wa uchumi.

KHADIJA KOMBO-PEMBA.   Watendaji wa Mahakama Kisiwani Pemba wametakiwa   kufanyakazi kwa uadilifu na uwajibikaji kwani wao ndio tegemeo kubwa   la wananchi   katika kupata haki zao. Akifungua warsha ya siku moja kwa Watendaji wa mahakama Kisiwani Pemba Jaji Mkaazi Pemba Mh. Ibrahim Mzee Ibrahim amesema watendaji hao ndio roho ya mahakama,   hivyo hawana budi kufanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa huku wakiwa tayari kukataa rushwa na uhujumu wa uchumi nchini. Kwa upande wao washauri waelekezi Khamis Kombo Mohammed kutoka ZAECA na Suleiman Omar Suleiman   kutoka Chuo cha Utawala wa Umma wamesema  kuna baadhi ya watendaji ambao si waadilifu hivyo huchukulia nafasi zao kama njia ya kudai rushwa hivyo hakuna budi kubadilika ili kuondokana na vitendo hivyo ambavyo vinaathari...
Kitaifa, Sheria

TAMWA-ZNZ, ZAFELA YAPONGEZA JESHI LA POLISI KWA KUMKAMATA MTUHUMIWA WA MAUWAJI ZANZIBAR

TAMWA-ZNZ, ZAFELA YAPONGEZA JESHI LA POLISI KWA KUMKAMATA MTUHUMIWA WA MAUWAJI JUMUIYA ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) vinalipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kuharakisha uchunguzi na kupatikana kwa mtuhumiwa wa kesi ya mauaji ya marehemu Khairat Juma Bakari ambae aliuawa kikatili katikati ya mwezi wa Mei, 2023. Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi Zanzibar lilitoa taarifa ya kukamatwa kwa mtuhumiwa Yusuf Ame Abubakar ambaye anatuhumiwa kwa mauaji ya Khairat Bakar yaliyotokea huko Mbuzini wilaya ya Magharibi “A” Unguja na kuripotiwa na vyombo vya habari tarehe 20 ya mwezi Mei 2023. ZAFELA na TAMWA-ZNZ inapenda kulishukuru Jeshi la Polisi kwa hatua hiyo muhimu na kuendelea kuliomba jeshi hilo kuharakisha pia ...
WATANO WAKAMATWA NA POLISI KWA WIZI KASKAZINI UNGUJA
Sheria

WATANO WAKAMATWA NA POLISI KWA WIZI KASKAZINI UNGUJA

NA OMAR HASSAN – ZANZIBAR  Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja limefanikiwa kuwakamata watu watano kwa tuhuma za  wizi wa waya wa umeme wenye thamani ya shilingi milioni 70 na wizi wa mafuta ya dizel madumu 20. Akizungumza na vyombo vya habari huko Ofisini kwake Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja Kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi Daniel Shila amesema Juni 3 mwaka huu majira ya saa 8.30 usiku watuhumiwa Said Juma Said (30) mkaazi wa Nyarugusu, Juma Khamis Juma (34) mkaazi wa Mahonda, Robert Simon Makala (38) mkaazi wa Kiwengwa na Juma Haji Omar (46) mkaazi wa Magogoni wanatuhumiwa kuiba waya wa umeme mita 1064 wenye thamani ya milioni 70 huko katika eneo la ujenzi wa Hoteli ya Zanzibar Wave Kiwengwa. Aidha Kamanda Shila ameeleza kuwa Juni 7 mwaka huu, saa ...