Thursday, December 26

Siasa

Mhe Hemed aendelea na ziara yake ya kuangalia uhai wa chama jimbo la Mtambwe kisiwani Pemba
Siasa

Mhe Hemed aendelea na ziara yake ya kuangalia uhai wa chama jimbo la Mtambwe kisiwani Pemba

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla, Viongozi mbali mbali na wanachama wa CCM wakila kiapo cha utii mara baada ya zoezi la kuwakabidhi kadi wanachama wapya waliojiunga CCM wakati wa ziara ya kuimarisha Chama Jimbo la Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema kuna kila sababu ya Jimbo la Mtambwe kubaki katika Ngome ya Chama cha Mapinduzi katika ngazi zote za Uongozi ifikapo Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.   Akizungumza na wana CCM na wananchi wa Jimbo la Mtambwe huko katika viwanja vya kisiwani Mhe. Hemed amesema Chama kinahitaji kuimarishwa na kusimamiwa vizuri katika Jimbo hilo kwa kuongeza nguvu za kuwashawishi wananchi wa Mtambwe ili waweze kuendele...
Kamati ya Siasa Jimbo la Ole imeridhishwa na Utendaji kazi wa Vuingozi wa jimbo hilo
Siasa

Kamati ya Siasa Jimbo la Ole imeridhishwa na Utendaji kazi wa Vuingozi wa jimbo hilo

Amina Ahmed Moh'd KAMATI ya Siasa Jimbo la Ole Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba imesema imeridhishwa na kasi ya maendeleo iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na viongozi wa Jimbo  hilo katika kuleta maendeleo  ya huduma bora kwa wananchi  ndani ya Jimbo hilo. Akizungumza na habari hizi  mara baada ya kumalizika ziara maalum ya kutembelea na kukagua miradi mbali mbali iliyotekelezwa na  mwakilishi Massoud Ali Muhammed  pamoja  Mbunge wa jimbo hilo Juma Hamad Omar. Mwenyekiti  wa kamati hiyo ambae pia ni Kiongozi wa Madiwani   Wilaya ya Chake Chake Hamad Abdalla Hamad  amesema  utekelezaji  wa miradi hiyo imeleta Tija na  Maendeleo  kwa Wananchi katika kurahisisha  huduma mbali mbali . Kwa upande wake Mbunge Wa Jimbo la Ole Juma Hamad Omar  amesema  lengo la kuzi...
VIONGOZI VYAMA VYA SIASA PEMBA WAJENGEWA UWEZO KUHUSU SERA YA JINSIA KATIKA VYAMA VYAO.
Siasa

VIONGOZI VYAMA VYA SIASA PEMBA WAJENGEWA UWEZO KUHUSU SERA YA JINSIA KATIKA VYAMA VYAO.

AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.  ZAIDI  ya Viongozi 15 kutoka vyama mbali mbali vya Siasa  kisiwani  Pemba wamepatiwa Mafunzo maalum   kujengewa uwezo juu ya Kuanzisha na kuifanyia  kazi Sera ya jinsia Katika Vyama Vyao. Mafunzo hayo ya Siku moja yaliondaliwa na Chama  cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na Jumuia ya Utetezi wa kijinsia  na Mazingira Pemba  PEGAO   yamefanyika Leo katika ukumbi wa Chama hicho Mkanjuni Chake Chake.  Akizungumza katika Mafunzo hayo Mratibu wa chama hicho Pemba Fat-hiya Mussa Said Amesema lengo la Mafunzo hayo kwa Viongozi wa vyama vya Siasa ni  kusaidia Kuongeza  ushiriki wa  wanawake Katika Demokrasia kwa kufuata Utaratibu maalum utakaotambulika kisheria, kusimamiwa pamoja na kuweza kutekelezwa  kupitia  Sera ya Ki...
Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa kusini Pemba toweni Elimu kwa viongozi wa ngazi mbali mbali
Siasa

Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa kusini Pemba toweni Elimu kwa viongozi wa ngazi mbali mbali

  HABIBA ZARALI, PEMBA MAKAMO Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi (CCM ) ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amewataka wajumbe wa Halmashauri kuu ya Mkoa wa kusini Pemba kutowa elimu kwa viongozi wa ngazi mbalimbali ili kila mmoja kuweza kujuwa na kutekeleza majukumu yake ipasavyo . Alisema viongozi ndio wenye jukumu la kuhakikisha wanatowa elimu ya kukijenga chama na kuleta mafanikio yanayohitajika na sio vyenginevyo. Kauli hiyo aliitowa katika ukumbi wa umoja ni nguvu Mkoani wakati akizungumza na viongozi wa chama cha Mapinduzi ikiwa ni siku yake ya mwanzo ya kichama  Mkoa wa Kusini Pemba. Makamo Mwenyekiti alisisitiza viongozi hao kuacha makundi katika chama na badala yake waandikishe wanachama wapya kwani bad...
Makamo mwenyekiti CCM azungumza na  wanachama wa chama cha Mapinduzi Pemba
Siasa

Makamo mwenyekiti CCM azungumza na wanachama wa chama cha Mapinduzi Pemba

NA ZUHURA JUMA, PEMBA MAKAMO Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM kuendelea kufanya kazi ya kukijenga chama, ili kuendelea kushika dola. Alisema kuwa, chama chochote cha siasa kina jukumu la kushika dola, hivyo kuna haja ya kujipanga kikamilifu kuanzia sasa ili kuhakikisha chama cha Mapinduzi CCM kinaendelea kushika dola siku zote. Akizungumza na wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba, Makamo huyo alisema kuwa, ni vyema kwa wanachama wakafanya kazi ya kukiimarisha chama cha CCM ili kuendelea kushinda katika chaguzi zote zinazofanyika kila baada ya miaka mitano. "Baada ya kumaliza uchaguzi kwenye chama chetu maana yake sasa, tunatakiwa tu...