Friday, December 27

Siasa

 Fedha za mfuko wa jimbo  kuweka uwazi wa matumizi yake  ili kuondosha migogoro 
Siasa

 Fedha za mfuko wa jimbo  kuweka uwazi wa matumizi yake  ili kuondosha migogoro 

NA ABDI SULEIMAN. WAJUMBE wa Kamati ya Maendeleo ya skuli ya Maandalizi na Msingi Tundauwa Wilaya ya Chake Chake, wamewataka wahasibu wanaosimamia fedha za mfuko wa jimbo za Mwakilishi na Mbunge, kuweka uwazi wa matumizi ya fedha hizo wakati wanapozipeleka katika miradi ya jamii. Wamesema uwazi huo utasaidia kujulikana na matumizi halisi ya fedha hizo, na kuondosha migogoro na mabishano pale matumizi yanapokua sio sahihi. Wajumbe wa kamati hiyo waliyaeleza hayo, wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayojengwa kupitia fedha za mfuko wa jimbo na mwakilishi wa jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake. Mwalimu Juma Maalim Khatib, alisema wakati wautekelezaji wa miradi, vizuri mambo ya fedha za mfuko huo zinapopelekwa katika miradi kuwekwa wazi juu ya matumizi yak...
Soko la mboga mboga na matunda Tondooni Pujini kujengwa la kisasa.
Siasa

Soko la mboga mboga na matunda Tondooni Pujini kujengwa la kisasa.

NA ABDI SULEIMAN. MWAKILISHI wa Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake Suleiman Massoud Makame, amesema kuwa suala la maendeleo kwenye serikali ya awamu ya nane hayana chama ni kwa ajili ya wananchi wote wa Zanzibar. Alisema wanachama wa CCM, ACT Wazalendo, CUF na vyama vyengine wote wananufaika na maendeleo yanayoletwa nchini, ikiwemo barabara, hospitali, skuli, maji safi na salama, umeme na masoko. Mwakilishi huyo aliyaeleza hayo, wakati akikagua maendeleo yaliyofikiwa ya soko la mboga mboga na matunda Tondooni Pujini jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake, wakati waziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo jimboni humo. Alisema bado dhamira yake iko pale pale ya kuhakikisha soko hilo, linamalizika kwa wakati na wananchi wanafanya biashara zao mbali mbali ndani. “Niliwa...
UWT wamkabidhi kadi ya uananchama Mama Mariam Mwinyi
Siasa

UWT wamkabidhi kadi ya uananchama Mama Mariam Mwinyi

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mariam Mwinyi amewahimiza Wanawake CCM, kupigania nafasi za maamuzi kwenye uongozi ili kuendelea kuwainua wanawake wasio na sauti na kuwasihi kamwe wasirudi nyuma kwa hatua waliopiga. Amesema amefurahishwa na kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na aliwataka waongeze juhudi katika kutetea maslahi ya mwanamke nchini. Mama Mariam Mwinyi aliyasema hayo alipozungumza na kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Amani Kichama, iliyofika Ofisini kwake Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Bi. Fransisca  Clement waliofika kwa lengo la kumkabidhi kadi ya uanachama wa (UWT). Aidha, ali...
Dk. Hussein  Mwinyi azindua tena Kamati ya Maridhiano baina ya Chama cha Mapinduzi na ACT Wazalendo.
Kitaifa, Siasa

Dk. Hussein Mwinyi azindua tena Kamati ya Maridhiano baina ya Chama cha Mapinduzi na ACT Wazalendo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameendelea kusisitiza dhamira yake njema ya kuiunganisha tena Zanzibar kuwa moja yenye amani, upendo, maridhiano na mshikamo. Ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alipozindua tena Kamati ya Maridhiano baina ya Chama cha Mapinduzi na ACT Wazalendo ifanyekazi pamoja kuendeleza amani iliyopo nchini. Alisema bado ana nia ya kuiendeleza Zanzibar kuwa moja bila kujali rangi, asili, imani za dini, au itikadi za kisiasa kama alivyoahidi kwa mara ya kwanza alipohutubia Baraza la Wawakilishi mwezi Novemba, 2022 juu ya dhamira yake ya kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar kuwa wamoja. Alisema mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 waliendeleza tena Serikali ya Umoja wa kitaifa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar kama il...