Sunday, November 24

Siasa

VIDEO: Mama  Maryam  Mwinyi amuombea kura DK. Hussein Ali Mwinyi.
Kitaifa, Siasa

VIDEO: Mama Maryam Mwinyi amuombea kura DK. Hussein Ali Mwinyi.

  Waswahili wanasema Mwanamme yeyote Yule ambaye amepiga hatua ya mafanikio basi ujue kuwa nyuma yake kuna mwanamke ambae amesaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kwa upatikanaji wa mafanikio hayo. Mama  Maryam  Mwinyi Mke wa Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi na yeye kwa upande wake anataka kuthibisha ukweli wa msemo huo kwani wakati wote hatua kwa hatua yuko sambamba na Dr. Hussein Mwinyi katika kuusaka Urais wa Zanzibar kupia tiket ya Chama cha Mapinduzi. Huko Katika kijiji cha Shumba Mjini Mama Maryam  alikutana na akina mama wa shehia hio ambapo bila ya ajizi aliwaomba akina  mama hao kumchagua Dr. Hussein Ali Mwinyi pamoja na wagombea wengine kupitia chama cha Mapinduzi ili waweze kupata ridhaa ya kuiongoza  Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitanoi jayo kwa leng...
Dk. Hussein Ali Mwinyi:  kama nikipata ridhaa ya kuwa rais wa Zanzibar, nitahakikisha kunatungwa sheria, ambayo itawawezesha wajane kupata haki zao stahili.
Biashara, Kitaifa, Sheria, Siasa, Wanawake & Watoto

Dk. Hussein Ali Mwinyi: kama nikipata ridhaa ya kuwa rais wa Zanzibar, nitahakikisha kunatungwa sheria, ambayo itawawezesha wajane kupata haki zao stahili.

NA MWANDISHI WETU, PEMBA .   MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kama akipata ridhaa ya kuwa rais wa Zanzibar, atahakikisha kunatungwa sheria, ambayo itawawezesha wajane kupata haki zao stahili, kama yalivyo makundi mengine. Alisema anaelewa changamoto kadhaa zinazowakumba wanawake hao, iwe kwa wale wanaoachwa au kufiwa na waume, kwa kukoseshwa haki zao na kutupiwa mzigo wa malezi na huduma kwa watoto. Mgombea huyo wa urais, aliyasema hayo ukumbi wa zamani wa baraza la Wawakilishi mjini Wete Pemba, alipokuza akizungumza na wanachama wa jumuiya ya wajane Zanzibar kwa upande wa Pemba. Alisema, anatambua kuwa Zanzibar lipo kundi kubwa la wajane ambalo linaendelea kuteseka na kuhangaika huku na kule na wale wanaume w...
ADC yalaani vitendo vya uvunjifu wa amani.
Kitaifa, Siasa

ADC yalaani vitendo vya uvunjifu wa amani.

CHAMA cha Alliance For Democratic Change (ADC), kimelaani vikali kauli zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa, ambazo zinaashiria uvunjifu wa amani nchini, huku wakivitaka vyombo vya ulinzi na usalama na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Jaji Mutungi kutokuvifumbia macho na kuvipuuza. Chama hicho kimesema kauli hizo za chokochoko hata mwaka 2001, zilikuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa siasa wakati wa kampeni, jambo ambalo mwisho wake zilipelekea vurugu na kusababisha taifa kuingia doa. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ADC Taifa, Omar Costantino Pweza wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari, huko katika ofisi ya Kanda ya ADC Wawi, kufuatia kujitokeza kwa viashiria vya uvunjifu wa amani Kisiwani Pemba. Mk...
Dk. Hussein Ali Mwinyi :Nitasimamia uwajibikaji na watakoshindwa nitawawajibisha.
Kitaifa, Siasa

Dk. Hussein Ali Mwinyi :Nitasimamia uwajibikaji na watakoshindwa nitawawajibisha.

NA HAJI NASSOR, PEMBA     NGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema iwapo wananchi wa Zanzibar watampa ridhaa ya kushika nafasi hiyo, atahakikisha, anasimamia uwajibikaji na watakoshindwa atawawajibisha, ili mafanikio ya kweli yapatikane. Alisema, hayo ndio kipaumbele chake cha kwanza mara atapomaliza kuapishwa, kwani mambo hayo ni miongoni mwa yanadhoofisha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii. Mgombea huyo wa urais, aliyasema hayo Jimbo la Gando wilaya Wete mkoa wa kaskazini Pemba, alipokuwa akizugumza na mamia ya wanaccm na wananchi wengine, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni wa chama hicho. Alisema kuwa, serikali atakayoiongoza hatopenda hata kidogo kuona ndani yake, mna watendaji wasiopenda...
Kitaifa, Siasa

VIDEO: Wagombea CCM jimbo la Pandani nao wanadi sera zao.

Mjumbe wa Halmashauri kuu  ya CCM Taifa Ramadhan Shaib Juma amewataka wana CCM na wananchi wote wapenda amani kuwachagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi na  kujitokeza kuendelea kuomba kura kwa wananchi wote bila ya kujali  itikadi za kisiasa, kwani  sera za CCM zinaelekeza  kuleta maendeleo kwa wananchi wote. Ndugu Ramadhan amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wana CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Pandani katika Mkutano wa kampeni wa Jimbo hilo huko shengejuu wakati wa kuwanadi wagombea wa nafasi ya Uwakilishi, ubunge pamoja na madiwani. Kwa upande wake Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Pandani ndugu Khamis Dadi Khamis amewaomba wana CCM wote na wapenda maendeleo kumchagua yeye pamoja na wagombea wote wa CCM wa Jimbo hilo ili waweze kuunganisha nguvu zao katika kukuza maen...