Sunday, November 24

Siasa

UWT KUANZISHA WASAIDIZI WA SHERIA.
Sheria, Siasa

UWT KUANZISHA WASAIDIZI WA SHERIA.

NA ABDI SULEIMAN. MWENYEKITI wa UWT Taifa Mary Pius Chatanda, amesema wanakusudia kuanzisha dawati la wasaidizi wa sheria katika ofisi za UWT, ili kuwasaidia wanawake na watoto wanaokumbana na changamoto za udhalilishaji na kuhitahi huduma za kisheria. Alisema dawati hilo litaanzishwa katika ofisi za UWT Tanzania nzima, ili kuwasaidia wanawake wanaokumbana na matatizo hayo kwa kuogopa kwenda mahakamani au kutokuwa na uwezo wakupata wakili. (more…)
“Tuyaenzi na kuyalinda  maridhiano  ya Zanzibar  ili kuwafanya watu wote kuwa kitu kimoja” Katibu Mkuu CUF
Siasa

“Tuyaenzi na kuyalinda  maridhiano  ya Zanzibar  ili kuwafanya watu wote kuwa kitu kimoja” Katibu Mkuu CUF

 NA FATMA HAMAD PEMBA. Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Hamad Massoud Hamad amewataka viongozi wenzake wa vyama vya siasa nchini kuyaenzi na kuyalinda  maridhiano  ya Zanzibar  ili kuwafanya watu wote kuwa kitu kimoja. Katibu huyo ametoa wito huo wakati akizungumza na wapenzi na wafuasi wa chama cha CUF  katika mkutano wake wa mwanzo tokea kuondolewa kwa zuio la mikutano ya hadhara na Rais  wa Jamuhuri ya Muungano  Samia Suluhu Hassan huko wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema kazi walioifanya viongozi wa Zanzibar  akiwemo marehemu maalimu Seif Sharif pamoja na rais mwinyi la kufanya mazungumzo na kuanzisha maridhiano ni jambo kubwa, hivyo niwajibu viongozi kuyaendelenza na kuyatunza maridhiano hayo yaendelee kudumu hapa Nchini. ''Tumekua tukishuhudia...
UWT YAWAPA ONYO WANAWAKE
Kitaifa, Siasa, Wanawake & Watoto

UWT YAWAPA ONYO WANAWAKE

NA MARYAM SALUM, PEMBA. MWENYEKITI wa UWT Taifa Mary Pius Chatanda amewataka wanawake wenzake kuacha tabia ya kuwanyanyasa  na kuwatelekeza watoto kwani hilo sio jambo la busara kwa jamii na hata mbele ya Mungu. Wito huo ulitolewa na Mwenyekiti huyo katika Kiwanja chakufurahishia watoto kilichopo Tibirinzi Chake Chake kwenye wiki ya siku ya mwanamke Duniani ambapo huadhimishwa kila ifikapo machi 8 ya mwaka. Alisema kuwa suala la malezi kwa  watoto sio la mzazi mmoja ni jukumu la kila mmoja ndani ya jamii ili kuondosha changamoto mbali mbali zinazoweza kujitokeza. Alieleza kuwa sio jambo la busara kwa mzazi kutupa mtoto ama kutelekeza mtoto kwa sababu tu yakukosa huduma ama mahitaji kutoka kwa mwenza wake. “Tusitupe watoto kwani hatujui hapo mbeleni mtoto huyo unaemtupa a...
DHAMIRA NJEMA TIBA YA KUIREJESHA HAIBA YA ZANZIBAR – MHE. OTHMAN.
Kitaifa, Siasa

DHAMIRA NJEMA TIBA YA KUIREJESHA HAIBA YA ZANZIBAR – MHE. OTHMAN.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman amesema Nchi ya Zanzibar haikupaswa kuwa kituo cha umasikini, bali ilistahili pahala bora zaidi kutokana na haiba ya heshima yake tangu asili. Mheshimiwa Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo leo akiwahutubia maelfu ya wafuasi, wanachama na wananchi, waliomiminika katika Mkutano wa Hadhara wa Chama chake, huko Tibirinzi-Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba. (more…)