WHVUM inapaswa kusimamia uchezaji wangoma za uchi katika maeneo ya hoteli za kitalii.
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
WAJUMBE wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wamesema kuwa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, inapaswa kusimamia uchezaji wangoma za uchi katika maeneo ya hoteli za kitalii, ili kunusuru kupotea kwa maadili ya kizanzibari.
Wamesema nchi ina uwekezaji wa hoteli mbali mbali na ngoma nyingi zimekua zikichezwa usiku uchi, jambo ambalo linaleta athari kubwa kwa jamii iliyozungukwa na hoteli hizo na taifa kwa ujumla.
Hayo yameelezwa na wajumbe wa kamati hiyo, wakati wakichangia taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya baraza la Sanaa, sensa ya filam na utamaduni, kipindi Cha robo ya kwanza kuanzia Julai hadi Septemba 2023, Kwa wajumbe wa kamati hiyo huko katika ukumbi wa wizara ya habari Gombani....