Mfuko wa Maendeleo ya Filamu wa DW Akademie kwa Tanzania na Uganda wakaribisha maombi
katika Kukuza Utengenezaji wa filamu kwa nchi za Kusini mwa Dunia.
Kuanzia Septemba 14, 2021, watengenezaji wa filamu kutoka Tanzania na Uganda wanaalikwa kuomba fedha za kuwezesha uendelezaji wa matayarisho ya utengenezaji wa filamu na kupata mafunzo yatakayotolewa na DW Akademie.
Shirika la maendeleo ya habari la Ujerumani la DW Akademie, linalenga watengenezaji wa filamu kutoka Uganda na Tanzania ambao tayari wametengeneza filamu moja au zaidi, na wangependa kupata misaada katika utayarishaji wa miradi yao mipya ya filamu. Ifikapo Januari 2022 waombaji hadi watano, kutoka kila nchi hizi mbili, watachaguliwa na majopo tofauti ya majaji, ili kupokea ruzuku inayoweza kufikia Euro 10,000, pamoja na ushauri kwa kipindi cha mwaka mmoja, ili kuwasaidia kuendeleza ubora wa miradi yao ya fil...