Mashindano ya vikundi vya sanaa yafanyika uwanja wa michezo Gombani
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
NA ABDI SULEIMAN.
WAZIRI wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Tabia Maulidi Mwita, amewataka wasanii wa vikundi vya sanaa Ksiiwani Pemba, kuhakikisha sanaa hiyo wanawarithisha vijana wao ili iweze kuendelea kudumu.
Alisema sanaa nyingi zimekua zikipotea kutokana na wazee kushindwa kuzirithisha kwa vijana wao, jambo ambalo linapelekea sanaa hizo kupotea siku hadi siku.
Waziri Tabia aliyaeleza hayo katika hutuba yake wakati wa mashindano ya vikundi vya sanaa Pemba, yaliyofanyika uwanja wa Michezo Gombani Chake Chake Pemba.
Aidha alisema Wizara itahakikisha inakamilisha yale yote yanayohitajika katika kuboresha sana za utamaduni zikiwemo ngoma za asili, ili ziweze kuendelea kubaki katika asili yake na kuris...