Sunday, November 24

Utamaduni

Waziri Mhe.Bashungwa Ameipongeza DSTV Kwa Kujali Maudhui ya Kitanzania Katika Kukuza Sanaa.
Michezo, Utamaduni

Waziri Mhe.Bashungwa Ameipongeza DSTV Kwa Kujali Maudhui ya Kitanzania Katika Kukuza Sanaa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Innocent Bashungwa ametoa pongezi kwa  Kampuni ya DSTV Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele  kusaidia Tasnia ya Filamu nchini kupitia Chaneli zao   Waziri Bashungwa amesema hayo alipokutana na  Viongozi wa DSTV leo Julai 5, 2021 Jijini Dar es Salaam ikiwa ni ziara ya kuendeleza  mahusiano kati ya Wizara na Kampuni hiyo “Mimi nawapongeza  DSTV kwa kuwa  mstari wa mbele katika kukuza sanaa yetu ukizingatia mmeweka Chaneli ya Maisha Magic Bongo kwaajili ya filamu na tamthiliya za kitanzania tu hii ina manufaa sana kwa wasanii wetu kama dada yangu Lamata hapa kaweza kujiajiri na kuwaajiri Watanzania wenzie wengi kama waandishi wa miswada, wapiga picha na wasanii kwa ujumla hii yote ni kutokana na DSTV kutoa mwanya kwa wasanii wetu kuon...
“MWANAMKE KAMATA FURSA DUNIA INAKUSUBIRI” Ufunguzi wa Kongamano la Ustaraab wa Wanawake Zanzibar
Kitaifa, Utamaduni

“MWANAMKE KAMATA FURSA DUNIA INAKUSUBIRI” Ufunguzi wa Kongamano la Ustaraab wa Wanawake Zanzibar

Mke wa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zainab Kombo Shaib akiskiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Wajane Zanzibar ( ZAWIO)Tabia Makame katika hafla ya Ufunguzi wa Kongamano la Ustaarabu wa Mwanamke  Ukumbi wa Sanaa Rahaleo  Zanzibar. Mwanaharakati wa masuala ya kijamii Raya Hamad Mchere akielezea maana ya ustaarabu wa Mwanamke katika Kongamano hilo hafla iliyofanyika  Ukumbi wa Sanaa Rahaleo  Mjini Zanzibar. Mjasiriamali Chiku Marzouk Ali  akielezea anavyofahamu  maana ya  Ustaarabu wa Mwanamke katika Kongamano  linalohusu Ustaarabu wa Mwanamke huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. Mjasiriamali  Isha Salim Hamad aliyevaa Mtandio (rangi Nyekundu ) akielezea anavyofahamu  maana ya  Ustaarabu wa Mwanamke katika Kongamano  linalohusu Ustaarabu wa Mwanamke huko Ukumbi ...
MASHINDANO ya elimu bila ya malipo Wilaya ya Wete
Michezo, Utamaduni

MASHINDANO ya elimu bila ya malipo Wilaya ya Wete

NA SAID ABDULRAHMAN.   MASHINDANO ya elimu bila ya malipo Wilaya ya Wete, yaliendelea tena mwishoni wiki lililopita kwa upande wa michezo ya sanaa na maigizo.   Mashindano hayo ambayo yalifanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Mchangamdogo, yaliweza kuzikutanisha Skuli zote msingi na Sekondari zilizomo katika Wilaya hiyo.   Katika ngarambe hizo Skuli ambazo zimeshinda nafasi ya kwanza na ya pili, zitaweza kuiwakilisha Wilaya ya Wete kwa ngazi ya Mkoa ambapo wataweza kushindana na mabingwa wenzao wa Wilaya ya Micheweni.   Michezo iliweza kushindaniwa ni pamoja na Ushairi, Utenzi, Wimbo, Tamthilia na mdahalo.   Kwa upande wa Ushairi, washindi ni Skuli ya msingi Kisiwani walipata alama 275 sawa na asilimia 91.66%, mshindi wa pili sk...
Mhe Hemed mgeni rasmi katika uzinduzi wa Vipindi vya kumbukumbu ya mambo ya kale vilivyopewa jina “SOGEA NIKUJUZE”
Biashara, Utamaduni

Mhe Hemed mgeni rasmi katika uzinduzi wa Vipindi vya kumbukumbu ya mambo ya kale vilivyopewa jina “SOGEA NIKUJUZE”

Makamu wa Pili wa Rais wa Rais wa Zanzibar akikabidhi vyeti pamoja na zawadi kwa washiriki waliosaidia kufanikisha hafla ya uzinduzi wa vipindi vilivyoandaliwa na Kampuni ya Mavips Pictures ambavyo vitarushwa hewani kwa Kushirkiana Mambo TV Swahili Kassim Abdi Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeahidi kuzipa Ushirikiano taasisi na kampuni binafsi zenye lengo la kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuiendeleza na kuitambulisha historia ya Zanzibar kwa lengo la kuimarisha utalii. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed  Suleiman Abdulla alieleza hayo wakati wa akizindua  vipindi vya  kumbukumbu ya mambo ya kale Zanzibar vilivyopewa jina (SOGEA NIKUJUZE) uzinduzi ambao uliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul...
WIZARA ya Utalii na Mambo ya kale imejipanga kurejesha michezo ya zamani ambayo kwa sasa imepotea.
Utamaduni

WIZARA ya Utalii na Mambo ya kale imejipanga kurejesha michezo ya zamani ambayo kwa sasa imepotea.

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA WIZARA ya Utalii na Mambo ya kale imejipanga kurejesha michezo ya zamani ambayo kwa sasa imepotea ili kuvutia watalii wa nje na ndani ya nchi. Akizungumza Mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika makumbusho yaliyopo mjini Chake Chake ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya makumbusho duniani, Afisa Mdhamini Wizara hiyo Zuhura Mgeni alisema, siku hiyo ni fursa adhimu katika kuutangaza utalii kwenye visiwa vyao. Alisema kuwa, katika kisiwa cha Pemba kuna vivutio mbali mbali vya utalii ambavyo vikiboreshwa ama kurejeshwa upya vitawavutia wageni kuingia na wenyeji, jambo ambalo litaongeza pato la nchi. Alisema, Wizara imejipanga katika kuhakikisha wanairejesha michezo ya zamani, ambayo wanaamini kwamba watavutia...