Wednesday, January 15

Utamaduni

RAIS DK. MWINYI AHUDHURIA TAARAB MAALUM YA MIAKA 59 YA MAPINDUZI
Kitaifa, Michezo, Utamaduni

RAIS DK. MWINYI AHUDHURIA TAARAB MAALUM YA MIAKA 59 YA MAPINDUZI

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi jana usiku alijumuika na wananchi na viongozi mbalimbali wa chama na serikali kwenye taarabu rasmi ya maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo. Taarabu hiyo ilitumbuizwa na vikundi viwili tofauti kikiwemo kikundi cha sanaa cha taifa pamoja na kikundi cha “Island Morden taarabu, maarufu kama Wajelajela” ilikua maalumu kwa kuyaenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 pamoja na kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa kazi kubwa aliyoifanya ndani kipindi cha miaka miwili ya uongozi kwa kuiletea Zanzibar maendeleo makubwa. Katika hafla hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa ndege, Zanzibar ulipambwa kwa vifijo na hoi...
Mhe Othman azindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Jozani Ghuba ya Chawa na Hifadhi Hai
Biashara, Kitaifa, MAZINGIRA, Utamaduni

Mhe Othman azindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Jozani Ghuba ya Chawa na Hifadhi Hai

MKOA WA KUSINI UNGUJA Makamu wa Kwanza  wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema  uzinduzi rasmi wa Hifadhi ya Taifa ya Jozani Ghuba ya Chawa na Hifadhi Hai ni  ufunguzi muhimu wa fursa nyingi zaidi za Kiuchumi, Kijamii na Kiikolojia hapa Zanzibar. Mhe. Othman ameyasema hayo huko Jozani wilaya ya Kusini Unguja alipozindua rasmi Hifadhi ya Taifa ya Jozani Ghuba ya Chawa na Hifadhi Hai, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za kutimia miaka 59 ya Mapinduzi ya Zazibar. Mhe. Othman ameitaka jamii wadau na washirika mbali mbali kuhakikisha kwamba hifadhi hiyo inalindwa ili iweze kutimiza malengo  malengo ya kuisaidia Zanzibar kuongeza pato kutokana na sekta ya utalii kwa wegeni wengi kuweza kutembelea msitu huo . Mhe. Makamu amefahamisha kwamba kwa mujibu wa wataalamu, Hi...
Kuhamasisha utumiaji wa lugha ya kiswahili kwa wageni na wenyeji kutasaidia kufanikisha mpango mkakati wa kitaifa wa kukuza na kuendeleza kiswahili nchini
Kitaifa, Utamaduni

Kuhamasisha utumiaji wa lugha ya kiswahili kwa wageni na wenyeji kutasaidia kufanikisha mpango mkakati wa kitaifa wa kukuza na kuendeleza kiswahili nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Fatma Hamad Rajab akiwahutubia wakufunzi waliyofika katika mafunzo ya Kiswahili kwa wageni  mara baada ya kuwasili  ukumbi wa Sanaa Mwanakwerekwe  mjini Zanzibar. Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili (BAKIZA) Dkt. Mwanahija Ali Juma akimkaribisha mgeni rasmin  wakati alipowasili katika mafunzo ya Kiswahili kwa wageni yaliyoandaliwa na baraza la kiwsahli huko ukumbi wa Mwanakwerekwe Mijini Zanzibar. (kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab (kushoto) Kamishina Idara ya Utamaduni Dkt. Omar Salum Mohammed. Daktari wa mashairi kutoka chakuwaza Issa Ali Issa akitumbuiza ushairi mara baada ya kuwasili mgeni rasmin katika mafunzo ya Kiswahili kwa wageni huko ukumbi wa Sa...