‘Khamis’ kisiwa kidogo kilichobeba historia ya Pemba
‘Khamis’ kisiwa kidogo kilichobeba historia ya Pemba
Utalii yakiibua kama kivutio kipya, kina ndege aina 12
NA HANIFA SALIM, PEMBA
Ni takribani dakika 25, kutoka katika ufukwe kwa bandari ya Tumbe, hadi kufikia kwenye kisiwa cha Ndege ‘Khamis’ kilichopo katika eneo la Tumbe ndani ya bahari ya Hindi.
Ilikuwa majira ya saa 3:00 asubuhi, boti iliyobeba maafisa wa wizara ya utalii na mambo ya kale, ikiwasili katika kisiwa Ndege kinachojulikana kwa jina la (kisiwa khamis).
Hali ya hewa ilikuwa ni ya mawingu mawingu, kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku mzima wa kuamkia siku hiyo, boti hiyo aina ya mashua, ilibeba takribani ya watu 30.
Katika msafara huo, jemedari wa Wilaya hiyo Mgeni Khatib Yahya amekiongozana na mwenye dhamana ya Wizara ya utalii na Mambo ya Kal...