UKODISHWAJI wa visiwa vidogo vidogo utasaidia upatikanaji wa soko la bidhaa.
NA ZUHURA JUMA, PEMBA
UKODISHWAJI wa visiwa vidogo vidogo utasaidia upatikanaji wa soko la uhakika kwa bidhaa wanazozalisha wajasiriamali kisiwani Pemba.
Wakizungumza na Zanzibarleo wananchi mbali mbali kisiwani Pemba walisema kuwa, visiwa vidogo vodogo vitakapokodishwa yatajengwa mahoteli ambapo wamiliki watahitaji bidhaa mbali mbali kutoka kwa wajasiriamali.
Walieleza, yatakapojengwa mahoteli katika visiwa hivyo wanaamini kuwa bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali zitapata soko kutokana na wamiliki wa mahoteli watahitaji bidhaa mbali mbali huku watalii wanapotembea pia watanunua bidhaa hizo.
Mmoja wa wakaazi wa Micheweni Pemba Hadia Hamad Shehe alieleza, Serikali na taasisi binafsi zinaimarisha vikundi vya wanawake na vijana katika shughuli za ujasiriamali, ingawa wanako...