Thursday, December 26

UTLII

Benki ya Exim Yaunga Mkono Jitihada za Rais Mwinyi, Wadau Kuchochea Kasi ya Utalii Zanzibar.
Biashara, UTLII

Benki ya Exim Yaunga Mkono Jitihada za Rais Mwinyi, Wadau Kuchochea Kasi ya Utalii Zanzibar.

Na Mukrim Mohammed Benki ya Exim Tanzania imesisitiza dhamira yake kuhudumia wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ndani na nje ya nchi  ili kuunga mkono na kwenda sambamba na kasi pamoja na dhamira ya serikali katika kuchochea ukuaji wa sekta hiyo muhimu. Afisa Mtendaji wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu alitoa ahadi hiyo mbele ya Raisi wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi alipotembelea banda la benki hiyo kwenye Mkutano wa pili wa wadau wa sekta utalii Zanzibar (Z -Summit) unaofanyika visiwani humo hii leo. Kwa mujibu wa Bw Matundu, kufuatia jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanywa na serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuendeleza sekta ya utalii, Benki ya Exim imewekeza zaidi katika kuwahudumia wadau wa sekta hiyo ili waweze kunufaika na jitihada hizo za serikali kupitia hudum...
PPC yaanza kuvitangaza vivutio vya Utalii Pemba.
hifdhi na utalii, UTLII

PPC yaanza kuvitangaza vivutio vya Utalii Pemba.

Yasema sababu na Uwezo wa kufanya hivyo wanao Kuunga mkono kauli ya Rais wakiwa kama waandishi  na Wananchi ni wajibu wao HABIBA ZARALI ,PEMBA Mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya ameahidi kuendelea kutowa elimu kwa wananchi wa Wiaya hiyo juu ya umuhimu wa Utalii na kuboresha vivutio vya utalii ndani ya maeneo yao. Alitowa ahadi hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari Pemba ‘PPC’ katika mahojiano maalum yaliyofanyika katika maeneo ya makumbusho ya Haroun site , Chwaka Tumbe wilayani humo. Alisema katika wilaya ya Micheweni kumebarikiwa na vivutio vingi vya utalii vinavyoendelea kukuwa siku hadi siku jambo ambalo ni faraja kubwa kwa wananchi na Serikali kwa ujumla katika kukuza Uchumi. “Zamani wilaya ya Micheweni suala la...
Dk. Mwinyi afungua  afungua tamasha la Fahari ya Zanzibar,  na maadhimisho ya mwaka  kwa taasisi ya ZEEA
UTLII

Dk. Mwinyi afungua  afungua tamasha la Fahari ya Zanzibar,  na maadhimisho ya mwaka  kwa taasisi ya ZEEA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amezitaka taasisi zote zinazohusiana na usimamizi wa sekta ya Utalii nchini, kuhakikisha wajasiriamali wa ndani wanapewa kipaumbale kunufaika na fursa zinazopatikana kwenye sekta ya utalii hususan masoko ya bidhaa wanazozalisha. Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipofungua tamasha la Fahari ya Zanzibar sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa taasisi ya Wakala wa Uwezeshaji wa nchi kiuchumi Zanzibar (ZEEA) kwenye hoteli ya Golden Tulip, Uwanja wa ndege Mkoa wa Mjini Magharibi. Alisema hali hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi zinazoweza kuzalishwa Zanzibar na kuimarisha soko la ndani kwa wajasiriamali wake. “Nazika taasisi zote zinazohusiana na us...
KAMISHNA WAKULYAMBA AITAKA MAKUMBUSHO YA TAIFA KUFANYA UTAFITI WA MALIKALE
Utamaduni, UTLII

KAMISHNA WAKULYAMBA AITAKA MAKUMBUSHO YA TAIFA KUFANYA UTAFITI WA MALIKALE

Naibu Katibu, Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Wakulyamba ametembelea maeneo ya  Malikale ya Mbuamaji na Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam na kuitaka Makumbusho ya Taifa la Tanzania kufanya utafiti zaidi juu ya malikale zote  zinazopatikana katika maeneo hayo. Kamishna Wakulyamba ametoa agizo hilo leo  alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayosimamiwa na Makumbusho ya Taifa. Amesema ni muhimu utafiti wa kina ufanyike ili kuweza kupata taarifa sahihi za malikale hizo, ambazo zitasaidia katika kuandaa ufasili wa malikale hizo. " Fanyeni utafiti na kuweka maelezo ili anayetembelea aweze kuelewa" Amesema Kamishna Wakulyamba. Naibu Katibu Mkuu ametembelea kituo cha taarifa na kumbukumbu M...