Friday, December 27

UTLII

NGWARE ni michezo wa asili ndani ya Wilaya ya Micheweni
Makala, Michezo, Utamaduni, UTLII

NGWARE ni michezo wa asili ndani ya Wilaya ya Micheweni

  NGWARE ni michezo wa asili ndani ya Wilaya ya Micheweni Wachezaji hujiandaa kwa kunywa mtindi Tayari umeshajizoelea mashabiki wengi ndani ya wilaya hiyo NA ABDI SULEIMAN, PEMBA NGWARE ni Kupinga mtu mtama naweza kusema hivyo kwa upande mmoja, upande wa pilia ni mchezo unaotumia miguu na mikono katika uchezaji wake. (more…)
Mradi wa heshimu bahari kutekelezwa Zanzibar
Kitaifa, MAZINGIRA, UTLII

Mradi wa heshimu bahari kutekelezwa Zanzibar

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA MKURUGENZI Mkaazi kutoka Shirika la misaada la Kimataifa la Marekani (USAID) Tanzania Craig Hart, amesema shirika hilo linaunga mkono shughuli zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samiia Suluh Hassana pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Husseina Ali Miwnyi, katika kuwapatia maendeleo wananchi wake. (more…)
WATALII WAFURAHISHWA NA AINA MBALIMBALI ZA UTALII TANZANIA
UTLII

WATALII WAFURAHISHWA NA AINA MBALIMBALI ZA UTALII TANZANIA

Na Kassim Nyaki, Ngorongoro. Watalii wanaotembelea vivutio vya Utalii nchini hususan eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wameendelea kuvutiwa na aina mbalimbali za shughuli za utalii zilizoko katika Hifadhi hiyo. Shughuli za utalii ambazo zinafanyika katika hifadhi ya Ngorongoro ni pamoja na utalii wa picha (Photographic tourism), utalii wa kutembea (walking safaris), Utalii wa akiolojia (archeological tourism) katika Bonde la Olduvai na Laetoli, utalii wa kupanda maputo angani (hot air balloon) na utalii wa kupanda milima (Mountain hiking) ambayo vyote vinapatikana katika hifadhi ya Ngorongoro. Bw. Remen Rudolff kutoka  Marekani ameelezea kufurahishwa na utalii wa picha katika bonde la Ngorongoro lenye umbo la kipekee la mandhari asilia yaliyopambwa na mtawanyiko wa wanyama na nd...
Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kujenga ukuta Kuunusuru mji wa karne ya 11 kuvamiwa na maji ya bahari
hifdhi na utalii, UTLII

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kujenga ukuta Kuunusuru mji wa karne ya 11 kuvamiwa na maji ya bahari

NA ABDI SULEIMAN. MRATIBU wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale Pemba Khamis Ali Juma, amesema mikakati mbali mbali inaendelea kuchukuliwa na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, kuhakikisha eneo la Mkumbuu haliendelei  kuvamiwa na maji ya chumvi, kwa kujengwa ukuta wenye urefu wa mita 500. Alisema ukuta huo utaweza kuzuwia mawimbi ya maji ya bahari kutokuendelea kuumega mji wa karne ya 11, ambao kwa sasa ndio uliobakia baada ya mji wa karne ya Kwanza (1) kuwa katikati ya maji ya chumvi na mji wa karne ya tisa (9) nao kuliwa. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko katika majengo ya kihistria Mkumbuu Wilaya ya Chake Chake, alisema ujenzi wa ukuta huo utaambatana na ukarabatari wa maeneo ya kihistoria na sehemu za huduma,  mradi wote ukigharimu Bilioni 2, 2,407,316,675....
WANANCHI WAVUTIWA NA UTALII IKOLOJIA
hifdhi na utalii, UTLII

WANANCHI WAVUTIWA NA UTALII IKOLOJIA

Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii hususani eneo la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambapo wamekuwa wakipata elimu kuhusu uhifadhi wa misitu na mazingira na ufugaji wa nyuki Hata hivyo Utalii Ikolojia umekuwa ni kivutio kikubwa kwa wananchi wanaotembelea maonesho haya ya Sabasaba ambapo kutokana na uhifadhi wa misitu unapelekea wananchi kupata maeneo mazuri ya kupumzika ambayo ni tofauti na mboga za wanyama zenye wanyama wakali. Akizungumza Meneja wa Mipango na Masoko - TFS,  Neema Mbise amesema kuwa Wakala inaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika Maonesho haya ya Sabasaba kuhusu uhifadhi , biashara ya mazao ya misitu na masuala ya Utalii Ikolojia ambapo wakifika watakutana na ofa mbalimbali za kutembelea maeneo ya vivutio ...