Wanawake wenye nia ya kugombea Uchaguzi mkuu 2025 watakiwa kujifunza kwa waliowatangulia
NA MWANDISHI WETU.
KATIKA kuhakikisha ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi unaongezeka, wanawake wenye ndoto za kugombea uongozi wameshauriwa kuanza kujifunza kutoka kwa wanawake wanasiasa waliowatangulia ili kuongeza ujasiri na uthubutu wa kukabiliana na vikwazo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Ushauri huo umetolewa na wanasiasa wanawake wakongwe katika mkutano wa jukwaa la wanawake na uongozi lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari WanawakeTanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) na Ubalozi wa Norway kwa lengo la kuwaunganisha wanawake wanasiasa kutoka vyama mbalimbali vya siasa Pemba kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo kuhusu ushiriki wao kwenye nafasi za uongozi na namna ya kukabiliana na vikwazo vinavyoweza kurejesha nyuma ufikiaji wa malengo ya wanawake kiuongoz...