WADAU wa vijana wakutana Pemba watakiwa kuwasilisha taarifa zao katika taasisi za vijana
NA ABDI SULEIMAN.
ASASI za Kiraia zinazofanya kazi na vijana zimetakiwa kuwasilisha taarifa zao za kazi katika taasisi ya Vijana ili serikali ifahamu kazi wanazozifanya katika kuwainua vijana katika harakati za kiuchumi.
Hayo yameelezwa na afisa Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba Salum Ubwa Nassor, wakati akifungua mkutano wa uratibu wa shughuli za wadau wa maendeleo ya Vijana uliowashirikisha wadau kutoka taasisi za kiraia na serikali na kufanyika mjini Chake Chake.
Alisema asasi hizo zinafanya kazi kubwa sana lakini hazionekani, hivyo wanapaswa kushirikiana na serikali ili zinapotokezea changamoto ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Aidha aliwataka wadau wa maendeleo ya vijana Pemba, kuzidisha mashirikiano kwa wizara na jumuiya za vijana ili kuwas...