MAKALA: Ramia, mwanamke aliepambania kujengwa barabara ya Sebuwatu, lengo lake ijegwe kwa kiwango cha lami
NA ZUHURA JUMA, PEMBA
Kwa watu wa Sebuwatu, kati ya kijiji chao na mji wa Wete Pemba, ni mafupi sana… karibu kilomita tatu.
Lakini muda ulikuwa unachukua muda mrefu kwa aliyetaka kwenda huko au kurudi kijini kutoka mji wa Wete.
Kuifanya safari hio kwa miguu au gari la ng’ombe ni kazi pevu, yenye sulubu na huwa ngumu zaidi kwa mtu aliyebeba mzigo kichwani au mkononi.
Kwa aina wajawazito ndio hatari kabisa, hiyo inatokana na njia kuwa mbaya sana na zaidi wakati wa mvua.
Kila kukicha wanakijiji walikuwa wanajiuliza shida hii walioishuhudia tokea wakiwa wadogo itakwisha lini na wao kuwa na usafiri mzuri, wa haraka na salama kama wanavijiji wengine wa kisiwa cha Pemba?
Tunaambiwa baada ya dhiki faraja na sasa matatizo waliokuwa nayo wanakijiji cha Sebuwatu ...