Profesa Mnyaa azindua Ofisi za Kikosi cha KMKM na Chuo Cha Mafunzo Wete.
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
WAZIRI wa Uchukuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amesema utekelezaji wa mradi wa Ofisi Kikosi cha KMKM na Chuo Cha Mafunzo Wete, ni jambo la faraja katika suala zima la kuimarisha ulinzi na usalama, katika ukanda huu kwa sababu utawezesha kupunguza biashara haramu za magendo mbali mbali.
Alisema ujenzi huo utasaidia kuzuia uharibifu wa mazingira ya bahari, pamoja na kuzuia uhamiaji haramu katika eneo hili, jambo ambalo litasaidia kuimarisha usalama wa Taifa na uchumi kwa ujumla.
Hayo yameelezwa katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Mohamed Mussa, mara baada ya kufungua Hanga, Ofisi za Utawala za KMKM na Ofisi ya Kamanda Mkuu zoni ya Pemba Chuo cha Mafunzo huko...