Vijana wametakiwa kutambua vyema kinachoendelea katika masuala kusimamisha Utawalaa bora
Na Maryam Talib – Pemba.
Ofisa Mdhamin Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Pemba Halima Khamis Ali aliwataka vijana kutambua vyema kinachoendelea katika masuala kusimamisha Utawalaa bora katika maeneo tofauti kwani vijana ndio nguvu kazi ya taifa kusudi kuwa mabalozi wazuri katika jamii zetu.
Aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano wa siku moja uliowashirikisha vijana 40 kutoka shehia tofauti za Wilaya Chake Chake uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala bora kisiwani Pemba.
Mdhamin huyo alisema mafunzo hayo ya Rshwa na utawala bora ,ajira yamefanyika kwa vijana kwani wao ndio wahusika katika maswala mengi vijana kwani taifa imara ni taifa lenye vijana wengi lakini wawe na uzalendo na uchun...