Sunday, November 24
DC Micheweni awataka akinamama kutumia uzazi wa mpango kuimarisha afya zao, watoto
afya

DC Micheweni awataka akinamama kutumia uzazi wa mpango kuimarisha afya zao, watoto

NA ZUHURA JUMA  - PEMBA MKUU wa Wilaya Micheweni Mgeni Khatib Yahya amewataka akina mama wa vijiji vya shehia ya Tumbe Mashariki kujiunga na uzazi wa mpango, ili kuwanyonyesha watoto wao kwa kipindi cha miaka miwili kamili kwa ajili ya kujenga familia bora. Akiuzungumza na wananchi wa vijiji hivyo katika uzinduzi wa utowaji wa elimu ya afya na lishe alisema, uzazi wa mpango ni muhimu katika makuzi bora ya mtoto na mama. Alisema kuwa, suala la uzazi wa mpango kwa akina mama ni jambo muhimu sana kutokana na hali zao, kwani linawafanya watoto kuwa na afya njema, akili nzuri pamoja na makuzi bora sambamba na yeye kuimarisha afya yake kwa kupata mapumziko. ‘’Mama anapopumzika baada ya kujifungua anapata muda wa kupumzika, hivyo afya yake inaimarika na mtoto anapata kukua vizuri,...
WAFUGAJI samaki Pemba wataka Mahakama yao
Biashara

WAFUGAJI samaki Pemba wataka Mahakama yao

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA. WAFUGAJI wa Samaki Kisiwani Pemba wamesema wakati umefika sasa na wao kuwa na mahakama yao maalumu, itakayoweza kuwatia hatiani wizi wanaoiba samaki kwenye mabwawa. (more…)
PPC kuvitangaza vivutio vya Utalii kISIWANI Pemba , Kuunga mkono kauli ya Rais wakiwa kama waandishi   ni wajibu wao.
Makala

PPC kuvitangaza vivutio vya Utalii kISIWANI Pemba , Kuunga mkono kauli ya Rais wakiwa kama waandishi   ni wajibu wao.

Na Maryam Talib – Pemba. HAKIKA kuweza nikujiwezesha hakuna kitu kinachokuja bila ya kujishuhulisha hayo ni maneno ya bwana  Hamad Salim mwenye umri wa miaka (65) alipoamua kuanzisha shamba lake la viungo lililopo sehemu moja inayopatikana Gando katika shehia ya Gando mkoa wa  kaskazini Pemba. Kilimo cha viungo ni fursa adhimu iliyopuuzwa na kufichika katika  Kisiwa cha Pemba ambayo kama ingetumiwa vyema na wakaazi wa kisiwa hichi ingekuwa na manufaa makubwa hasa hasa kwa  utalii wa ndani  na kwa wananchi wa kawaida . Hata hivyo kuna fursa moja muhimu iliyofichika kwa wakaazi wa kisiwa cha Pemba ambayo takribani miaka saba sasa anaitumia Bwana Hamad Salim wa Gando nayo ni ya kilimo cha viungo ikiwamo kilimo cha vanilla, hiliki, midalasini, tangawizi, majano, pilipili manga na ...