Friday, November 1
WANANCHI wa Kijiji cha Kibumbwi neema imeanza kuwaangukia
Kitaifa

WANANCHI wa Kijiji cha Kibumbwi neema imeanza kuwaangukia

KIU ya Maendeleo pamoja na upatikanaji wa huduma za msingi ya Kijamii walizonazo Wananchi wa Kijiji cha Kibumbwi mbayo ni changamoto ya muda mrefu imeonyesha njia ya kupata Muarubaini kufuatia ziara maalum ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdullla aliyoifanya kujua kero zinazowakabili Wananchi hao. Muarubaini huo umepatikana kufuatia Wakuu wa Taasisi zinazosimamia huduma za Maji safi na salama, Umeme, Afya, Elimu pamoja na Miundombunu ya Mawasiliano ya Bara bara kuahidi mbele ya Mheshimiwa Hemedi kwamba huduma hizo  zitafikishwa katika Kijiji hicho ndani ya Miezi Mitatu kuanzia sasa. Mmoja wa Wananchi wa Kijiji hicho ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Bwana Mkombe Juma Khamis alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba wamepata matumaini makubwa k...
VIDEO: Wakulima waanza kunufaika na mbegu za muhogo aina ya  kizimbani pamoja na viazi mayai.
Biashara, Kitaifa

VIDEO: Wakulima waanza kunufaika na mbegu za muhogo aina ya kizimbani pamoja na viazi mayai.

  Wakulima wa kilimo cha muhogo na viazi  katika Shehiya  ya Mbuzini Chake Chake wameanza kunufaika na mbegu za muhogo aina ya kizimbani pamoja na viazi mayai ambazo zimefanyiwa utafiti na Idara ya Utafiti Kisiwani Pemba, Akizungumza na Waandishi wa habari wakati walipokuwa katika ziara ya kuwatembelea  wakulima hao ili kuona matokeo ya utafiti wa mbegu hizo Mmoja kati ya wakulima hao  Bibi Fatma Bakar Hamad amesema kwa kipindi cha miaka minne sasa tokea kuanza kupanda mbegu hizo amekuwa akipata mazao hayo kwa wingi na kuleta tofauti kubwa katika miaka yote alioanza kulima kilimo hicho. Naye  Mkuu wa utafiti wa zari Pemba ,Khatib Bakar Haji amesema baada ya  utafiti huo mbegu hizo zimebainika kuwa na sifa ya kustahamili ukame lakini pia zinatoa mazao kwa wingi na kupunguz...
WAANDISHI wa habari wametakiwa kufikiria mbinu au njia zitakazotumika kuleta amani nchini
Kitaifa

WAANDISHI wa habari wametakiwa kufikiria mbinu au njia zitakazotumika kuleta amani nchini

WAANDISHI wa habari wametakiwa kufikiria mbinu au njia mbali mbali ambazo watazitumia kuleta amani nchini, pamoja na kumaliza machafuko yanayoendelea duniani kwa kutumia mitandao ya kijamii. Hayo yameelezwa na aliyekua Afisa Mdhamini ya Habari utalii na Mambo ya Kale Pemba Khatib Juma Mjaja, wakati alipokua akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari Pemba, juu ya kushajihisha masuala ya amani na mijadala ya kijamii inayohusiana na upatikanaji wa haki baada ya uchaguzi Mkuu mkutano ulifanyika Mjini Chake Chake. Alisema kalamu za waandishi wa habari zinafika mbali iwapo wataweza kuzitumia, kwa kuandika taarifa mbali mbali zinazohusiana na amani na kuzisambaza katika miatandao ya Kijamii. Alisema tokea mwaka 2010 dunia imeingia katika machafuko makubwa, machafuko ambayo bado y...
Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wametakiwa kujikita katika kuandika habari  za mambo yaliyofanyiwa utafiti
Kitaifa

Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wametakiwa kujikita katika kuandika habari za mambo yaliyofanyiwa utafiti

  Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wametakiwa kujikita katika kuandika habari  za mambo yaliyofanyiwa utafiti ili jamii iweze kufahamu matokeo ya tafiti mbali mbali zinazofanywa nchini  kwa maslahi yao na Taifa kwa  ujumla. Akiwasilisha mada juu ya mbinu za Uandishi wa habari za Utafiti Dk. Ali Uki huko katika ukumbi wa maabara ya afya ya jamii Wawi amesema katika nchi huwa kuna fanywa tafiti mbali mbali   lakini  matokeo yake hayawafikii  wananchi. Amesema ili taarifa hizo ziweze  kuifikia jamii ni lazima waandishi wa habari  wawe karibu na watafiti  ili waweze kupata habari hizo na kuzifikisha kwa jamii kwa lugha ambayo wataweza kuifahamu kwa urahisi. Kwa upande wake Mkurugenzi  Idara ya menejimenti ya maarifa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dk. Bunini Manyi...
Waziri Ummy Ali Mwalimu akutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman
Kitaifa

Waziri Ummy Ali Mwalimu akutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman

Na Othman Khamis, OMPR Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman alisema katika suala zima la kuendelea kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchini ipo haja kwa Wataalamu wa Sekta za Mazingira Nchini kuangalia kwa kina uvamizi wa Maji ya Bahari yanayoendelea kukiathiri Kijiji cha Sipwese kiliopo Mkoa Kusini Pemba. Alisema Wananchi wa Kijiji hicho  hivi sasa wanaendelea kupata usumbufu mkubwa kutokana na sehemu wanayovukia kwenda upande wa Vijiji Jirani kuvamiwa na mmong’onyoko kukubwa wa ardhi unaosababishwa na kasi ya Maji ya bahari na kuhatarisha pia maisha ya Watoto wanaokwenda Skuli. Mheshimiwa Hemed Suleiman alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayesimamia masuala ya Muungano na Mazingira wa Serikali ya Jamuhuri ya Mu...