Friday, November 1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa  Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu afanya ziara  visiwani Zanzibar
Kitaifa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu afanya ziara visiwani Zanzibar

Na Lulu Mussa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Ummy Mwalimu amesema watanzania wote wanao wajibu wa kujivunia matunda ya Muungano ikiwa ni pamoja na miradi ya Maendeleo inayotekekezwa pande zote mbili za Muungano.   Akiwa visiwani Zanzibar katika siku yake ya pili ya ziara ya kikazi, Waziri Ummy ametembelea miradi ya TASAF na MIVARF ikiwa ni pamoja na Kituo cha Afya Kianga, Bwalo la Wanafunzi na Soko la Mbogamboga la Kinyasini.   Amesema pamoja na changamoto zilizopo zipo fursa kwa Watanzania kujiletea maendeleo na ustawi wao, kwa kuwa kuwepo kwa fursa hizo kumeleta tashwishi na matarajio makubwa kwa wananchi katika kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na kuchochea mafanikio katika maeneo mengine kwa maslahi ya Taifa   ...
TRA yakusanya Bil, 2,469,061,394.70  kwa mwezi wa  July – Novemba 2020.
Biashara, Kitaifa

TRA yakusanya Bil, 2,469,061,394.70 kwa mwezi wa July – Novemba 2020.

  MARYAM SALUM, PEMBA Jumla ya Tshs Bil, 2,469,061,394.70  zimekusanywa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Pemba sawa na asilimia 61, ikiwa makusanyo ya miezi 5 kuanzia July hadi Novemba 2020. Akiwasilisha  ripoti   hiyo, Ofisa mdhamini Idara ya Forodha Pemba, Yussuf Haji , kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais fedha na mipango  Jamal Kassim Ali  kwenye ziara yake aliyoifanya hivi karibuni Kisiwani humo. Alisema malengo ya makusanyo katika kipindi hicho ni Tshs 4,054,181,414.00 ambayo hayajafikiwa kwa sababu mbali mbali ikiwemo hofu ya wafanyabiashara kipindi cha uchaguzi mkuu. Alieleza  kuwa makusanyo ya kodi mwaka wa fedha uliopita 2019/2020 Mamlaka hiyo Pemba ilipangiwa kukusanya Tshs 7,990,155,250.50, ambapo iliweza kukusanya Tshs 7,289,195,658.58 sawa na asilimia 9...
Kitaifa

MBUNGE ataka kamati ya ufuatiliaji

  MBUNGE wa Jimbo la Kojani Wilaya , amewataka wasimamizi wa mpango shirikishi wa shehia ya Kiuyu Kigogoni kuhakikisha wanaunda kamati ya ufuatiliaji na Tathmini, ili kuona kilichopangwa kinafanyika kwa wakati muwafaka. Alisema kamati hiyo itaweza kuwakumbusha viongozi wanaosimamia mpango kuwa, kama kutakua na vipaombele havijatekelezwa na vilipangwa kufanyika. Hayo aliyaeleza wakati wakikao cha uwasilishaji wa Vipaombele vya mpango shirikishi wa shehia hiyo, mkutano uliofanyika kiuyu kigongoni Wilaya ya Wete. Alisema vipaombele vilivyoibuliwa vya afya, kilimo na elimu ni vipaombele muhimu sana kwa shehia hiyo, hivyo kamati hiyo inapaswa kuhakikisha vinatekelezwa kwa wakati kwa kushirikiana na taasisi husika. “Hongereni sana taasisi ya Milele Zanzibar Foundation kat...
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi awasimamisha kazi watumishi wa Serikali.
Kitaifa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi awasimamisha kazi watumishi wa Serikali.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemsimamisha kazi Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Sabra Issa Machano na watendaji wengine  kwa tuhuma za kuhusika na makosa mbali mbali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya Serikali. Dk. Mwinyi ametoa kauli ya kuwasimamisha watendaji hao  wakati alipozungumza na Viongozi na watendaji wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) katika ukumbi wa taasisi hiyo uliopo Victoria Garden,  Vuga Jijini hapa. Watendaji wengine waliohusika na hatua hiyo ni pamoja na Ramadhani Abdalla Ali pamoja na watendaji wa Kamati nzima ya Uratibu wa mradi wa Huduma za Jamii Mijini (ZUSP) kutoka Wizara ya Fedha. Alisema amechukua uamuzi wa kumsimamisha kazi Mkurugenzi...
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesaini makubaliano ya kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania
Kitaifa, Sheria

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesaini makubaliano ya kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania

  DODOMA, 23/12/2020 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesaini makubaliano ya kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania kwa lengo la kupanua wigo wa kuelimisha jamii na chama hicho kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na majanga, makubaliano hayo yamefanyika Jijini Dodoma mapema leo asubuhi. Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo, Skauti Mkuu, Mwantumu Mahiza alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa wimbi la moto kwenye shule na katika jamii. “Kazi ya chama cha Skauti ni kusaidia watu na viumbe na kuhakikisha nchi inakuwa na amani na salama kwa kuishi. Tulipoona majanga ya moto yanajitokeza kwenye shule na makazi ya watu, Skauti tukaona kuna haja ya kushirikiana na chombo cha kisheria. “Skauti tumeshiriki kwenye mambo mengi ya Uokoaji, tulikuwa tunafa...