Friday, November 1
Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ameongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi
Kitaifa, Siasa

Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ameongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi

RAIS Dk. Hussein Ali Mwinyi leo ameongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi akiwa Mwenyekiti wa Kikao hicho tokea achaguliwe kwa kishindo kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu 2020. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Baraza la Mapinduzi Ikulu Jijiji Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla. Wengine ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mawaziri, pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dk. Mwinyi Talib Haji. Rais Dk. Hussein mwinyi, alikifungua kikao hicho na kukiongoza...
MWAKILISHI wa jimbo la Ziwani ameipongeza taasisi ya  Milele Zanzibar Foundation.
Kitaifa

MWAKILISHI wa jimbo la Ziwani ameipongeza taasisi ya Milele Zanzibar Foundation.

NA SAID ABRAHAMAN.   MWAKILISHI wa jimbo la Ziwani Wilaya ya Chake Chake Suleiman Makame Ali, ameipongeza taasisi ya  Milele Zanzibar Foundation kutokana na juhudi zake za kuwaletea wanachi wa Zanzibar maendeleo.   Alisema kuwa Milele ni taasisi moja wapo ambayo imekuwa ikifanya kazi, kubwa ya kusaidia jamii katika kuharakisha maendeleo yao.   Makame aliyasema huko katika Kijiji cha Michungwani Shehia ya Michungwani, Wilaya ya Chake Chake wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Shehia hiyo   Mwakilishi huyo aliwataka wananchi hao kushirikiana na taasisi hiyo, katika kuhakikisha yale yote ambayo wameyapanga katika mpango wao shirikishi wa Shehia, yanafanyika bila ya pingamizi yeyote.   Sambamba na hayo alieleza kuwa atahakikisha ...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Kitaifa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Na Lulu Musa Waziri Ummy Mwalimu amefanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharrif Hamad Chukwani Zanzibar. Mhe. Hamad amesisitiza umuhimu wa Wizara zenye hoja za Muungano kukutana na kutafuta suluhu ya mapema na kuhamasisha  Wizara zisizo na hoja kukutana pia kwa lengo la kudumisha undugu baina ya  Tanzania bara na Tanzania Zanzibar. “Nashauri na kusisitiza Wizara zinazoshabihiana zikutane na kuhakikisha hoja zinazopatiwa ufumbuzi zitekelezwe ipasavyo” alisisitiza Maalimu Seif Sharif Hamad. Waziri Ummy Mwalimu yuko visiwani Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na hapo kesho atatembelea miradi ya Muungano inayotekelezwa pande zote mbili.
Makamu wa Pili wa Rais, Mhe Hemed amsimamisha kazi Afisa wa Idara ya Ustawi wa Jamii akiyekaidi agizo lake
Kitaifa, Wanawake & Watoto

Makamu wa Pili wa Rais, Mhe Hemed amsimamisha kazi Afisa wa Idara ya Ustawi wa Jamii akiyekaidi agizo lake

Na Othman Khamis, OMPR Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla amemuamuru Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto kumsimamisha Kazi mara Moja Afisa wa Idara ya Ustawi wa Jamii anayehusika na utoaji wa Kibali kwa ajili ya Uendeshaji wa Huduma za Watoto Yatima kwa kosa la kudharau Wito. Mheshimiwa Hemed alitoa agizo hilo alipofanya ziara fupi ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Majengo ya Watoto Mayatima hapo katika Mtaa wa Jumbi Wilaya ya Kati na kutokukuta Afisa yeyote wa Idara hiyo katika eneo hilo licha ya kupewa taarifa ya ziara hiyo mapema asubuhi. Alisema hicho ni kitendo cha dharau kilichoonyeshwa na Mtumishi huyo wa Idara ya Ustawi wa Jamii kwa vile hadi inamalizika ziara hiyo hakuna sababu zozote zilizowasilishwa kwa kutokuw...
RC Kaskazini asifu juhudi za mbunge kusaidia jamii
Kitaifa

RC Kaskazini asifu juhudi za mbunge kusaidia jamii

MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib, amesifu juhudi za wananchi wa Kizimbani wilaya ya Wete za kuanzisha ujenzi wa madrasa ya kur-ani, ili watoto wao wapate elimu ya dini ya kiislamu karibu na mazingira wanayoishi.   Alisema suala hilo ni jambo jema ambalo litawasaidia kwa kiasi kikubwa watoto kufuata elimu hiyo masafa marefu, huku akiahidi kusimamia ujenzi wa madarasa hiyo inakamilika na watoto wanaweza kusoma kwa bidii.   Salama alisema hayo kwenye ujenzi wa madrasa hiyo Kizimbani, wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mifuko 15 ya saruji na shilingi laki moja na elfu hamsini za mawe (150,000/=) msaada uliotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Wanawake Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Asia Sharif Omar.   Alisema kuwepo kwa madrasa hiyo itawas...